loader
Dstv Habarileo  Mobile
Shahidi asema hofu na woga ulimfanya asaini maelezo

Shahidi asema hofu na woga ulimfanya asaini maelezo

MSHITAKIWA katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu, Mohamed Ling’wenya ameieleza Mahakama Kuu divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuwa alisaini karatasi ya maelezo yake kutokana na hofu na woga baada ya kupata mateso akiwa Kituo cha Polisi Moshi.

Lingw’enya alidai hayo mbele ya Jaji Joachim Tiganga wakati akitoa ushahidi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili. Akiongozwa na Wakili Dickson Matata, alidai kuwa yeye alikuwa mwanajeshi Kikosi cha Makomandoo 92 KJ kazi ambayo aliacha mwaka 2017 na kwenda kufanya kazi katika kampuni ya Kusaga kokoto Mkoa wa Mtwara.

Shahidi huyo wa kwanza upande wa utetezi alidai aliacha kazi hiyo baada ya kupigiwa simu na Luteni Denis Urio ya kumlinda Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye ni shahidi wa nne katika kesi hiyo. Alidai Agosti 5, 2020 akiwa Moshi maeneo ya Rau Madukani yeye na Adam Kusekwa walivamiwa na polisi zaidi ya wanane na kupelekwa kituo cha Polisi Moshi na baadhi ya askari hao ni Ramadhan Kingai na Omary Mahita.

Alidai kuwa Agosti 6 mwaka jana akiwa amefungwa kitambaa machoni alipandishwa kwenye gari na kuanza safari na baadaye alikuja kugundua wameshafika Dar es Salaam safari ambayo ilianza jioni hadi alfajiri. Pia alidai wakati wa safari hiyo alipokuwa akitaka kuinua shingo alikandamizwa chini akielezwa kuwa hakuna kunyanyua kichwa na kwamba alikuwa kama mateka.

Alidai alifunguliwa kitambaa alichofungwa wakati akiwa mahabusu, alipouliza watu wengine walimweleza hapo ni Kituo cha Polisi Tazara na mahabusu wenzake walimweleza kuwa kituoni hapo hupelekwa watu wenye makosa ya ugaidi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b08defcfb4fbb35b20fdfd28c2208901.jpeg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Na Francisca Emmanuel

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi