loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waipongeza serikali kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito

Waipongeza serikali kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito

WADAU wa elimu wameipongeza serikali kwa kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kurudi shuleni ndani ya miaka miwili baada ya kukatisha masomo. Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako alitangaza uamuzi huo wa serikali juzi jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Rose Reuben alisema jana kuwa, uamuzi wa serikali ni jibu kwa wadau wa masuala ya haki za wanawake. Alisema wasichana wanaopata ujauzito shuleni wamekuwa wakikwama kuendelea na masomo licha ya kuwa wapo waliopewa ujauzito kwa kubakwa.

“Serikali imefanya yale ambayo wanawake wamekuwa wakipigania kwa miaka mingi hapa nchini, wanawake wamekuwa wakisisitiza kuhusiana na wasichana kurejea kusoma licha ya kupewa mimba kwa kuwa kwanza hiyo ni kati ya haki zao za msingi.”

“Lakini niwasihi wazazi na walezi kuhakikisha wanaendelea kulinda haki za wasichana dhidi ya matukio yanayoweza kuwasababishia kupata mimba, hapa namaanisha kuwa siyo sababu ya kuwa wanafunzi wakipewa mimba wanaruhusiwa kusoma basi ndiyo waone ni sawa kwa wanafunzi hao kuzaa,” alisema.

Mkurugenzi wa Shirika la Bright Jamii Initiative, Irene Fugara alisema uamuzi wa serikali ni sahihi na utakaokuwa na manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Alisema vipaji na uwezo wa kimasomo wa wanafunzi wengi nchini vimekuwa vikiathirika kutokana na zuio la kuendelea na masomo kutokana na ujauzito. Alisema wananchi na jamii kwa ujumla wanapaswa kushirikiana na serikali kuhakikisha ruhusa hiyo ya serikali haisababishi kuendelea kupatikana kwa mimba nyingi za wanafunzi. Mkurugenzi wa Shirika la Elimu na Ubunifu (Tedi), Grolia Anderson alisema elimu kwa wasichana ni kitu muhimu kisichotakiwa kufanyiwa mzaha na kuwa uamuzi wa serikali wa kuwarejesha darasani wasichana waliopata mimba ni kitu kinachopaswa kupongezwa.

“Hakika hiki ni kitu muhimu na cha kupongezwa kwa kuwa kwanza serikali imeonesha nia ya dhati ya kuwasaidia wanafunzi hao kusoma tena, hakukuwa na sababu ya kuwaacha wakae nyumbani sababu ya mimba wakati wanao uwezo wa kusoma na kusimama tena na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeona hilo,’’ alisema.

Mkurugenzi wa shirika linalosaidia haki za watoto mkoani Tanga katika kata za Maweni na Pongwe katika shule 12, Sophia Byanaku alisema ni muda sasa wa suala hilo kuwekwa kisheria ili hata miaka ijayo iwe ni sawa kwa mtoto wa kike kuendelea kuruhusiwa kusoma.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/bf8d3d6ff020257cbd0e779ee8c4b94f.jpeg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Na Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi