loader
Dstv Habarileo  Mobile
Benki zajiandaa kushusha riba

Benki zajiandaa kushusha riba

UMOJA wa Benki Tanzania umesema hivi karibuni benki zitaanza kutangaza punguzo la riba za mikopo. Mwenyekiti wa Umoja huo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmalik Nsekela alisema hayo jana Dodoma wakati wa mkutano wa 20 wa taasisi za fedha.

Nsekela alisema benki zitatekeleza agizo la Benki Kuu Tanzania (BoT) kwa kutangaza punguzo la riba ili kutoa fursa kwa sekta binafsi ikope na kuwekeza kukuza uchumi.

Alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza diplomasia kati ya Tanzania na nchi nyingine hivyo kuzivutia nchi nyingine zilete miradi nchini. Nsekela alisema sekta ya fedha imejipanga kukuza uchumi kidijiti kwa kuwafikia Watanzania wengi zaidi na kutoa huduma bora.

Katika mkutano huo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alisema pamoja na wananchi kutoa kodi, kukopa fedha benki kutokana na kushuka riba wanatakiwa fedha hizo wazifikishe benki. Mwigulu alisema wananchi wanatakiwa kuzitumia benki kuweka fedha kwa kufanya hivyo watakuwa wanakuza uchumi badala ya kuweka fedha hizo kwenye vyungu au kufukia chini.

Aliwataka wafanyabiashara wanapokopa benki walipe madeni. Alishukuru Shirika la Fedha Duniani kwa kutoa mkopo wa sh trilioni 1.3 kwa riba nafuu ambazo zinakwenda kusaidia kutenda miujiza katika maisha ya watu.

Dk Mwigulu alizitaka benki kuwa na ubunifu katika kuongeza kasi na kupunguza riba ili sekta binafsi itumie fedha hizo kuongeza mikopo kwa sekta binafsi kukopa fedha na kuwekeza hasa katika sekta muhimu kama kilimo, mifugo na uvuvi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/41c65c56251bfb2dde3e0e296755d0a1.jpeg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Na Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi