loader
KMKM mabingwa riadha Z’bar

KMKM mabingwa riadha Z’bar

TIMU ya Riadha ya Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo KMKM, imetwaa ubingwa wa Zanzibar katika michuano iliyomalizika jana mjini hapa.

KMKM ilishika nafasi hiyo baada ya kuwatupa ndugu zao wa JKU ambao walishika nafasi ya pili na kaka zao Nyuki walishika nafasi ya tatu.

Bingwa huyo ambae aliondoka na kombe la kitita cha Sh 700,000 alipata medali 31 zikiwemo za dhahabu 12, fedha 10 na shaba tisa. Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Kamati ya Ufundi ya Chama cha Riadha Zanzibar (ZAA) Faida Salmini Juma, alisema JKU ambao ni washindi wa pili walipata medali tisa za dhahabu, 12 fedha na shaba tisa.

Kwa upande wa timu ya Nyuki walioshika nafasi ya tatu, walipata medali sita za dhahabu, fedha mbili na shaba tano. Mgeni rasmi katika michuano hiyo alikuwa Katibu wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) Hussein Ahmada ambae alikabidhi zawadi kwa washindi hao.

Mshindi wa pili alipata kikombe na shilingi 500,000 na wa tatu akaondoka na kikombe kidogo na shilingi 300,000. Katika mashindano hayo timu ya Mafunzo ilitangazwa kuwa timu yenye nidhamu na kukabidhiwa Sh 100,000.

Mbali na timu hizo, nyingine zilizoshiriki michuano hiyo ni Polisi, Kidoti, Chemchem, Lumumba, Kidoti, MUKIJOPE na Uhamiaji.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/a4eb923d6f7a48cf9bca69777e670524.jpeg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi