loader
Saba wafa kwa kula kasa, Dk Mwinyi aomboleza

Saba wafa kwa kula kasa, Dk Mwinyi aomboleza

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za watu waliofa baada ya kula samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu katika kijiji cha Msuka Taponi, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mkuu wa Mkoa huo, Salama Mbarouk Khatib alisema hadi jana mchana watu saba walikuwa wameaga dunia. Khatib alisema waliodhurika ni kutoka familia tofauti na kwamba walikula kasa huyo Alhamisi na Ijumaa iliyopita. Alisema watu wawili walipoteza maisha kabla ya kufikishwa hospitali.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Juma Sadi alisema watu watatu walipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitali ya Micheweni na akataja majina yao kuwa ni Asma Said, Shafiii Ismail na Firdaus Ismail. Alisema daktari Omar Zubeir aliwapokea watu hao wakiwa wamepoteza nguvu kwa kuharisha na kutapika. Wavuvi wa vijiji vya Msuka, Tumbe na wingwi vilivyo jirani na Mombasa nchini Kenya ni maarufu kwa uvuvi wa kasa.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupitia idara ya maendeleo ya uvuvi imepiga marufuku uvuvi wa samaki aina ya kasa kutokana na tishio la kutoweka duniani. Kuna zaidi ya aina saba za kasa akiwemo duvi asiyefaa kuliwa na mwanadamu kwa kuwa ana sumu kali. Khatib alisema watu wawili waliaga dunia jana, 34 walikuwa bado wamelazwa hospitali, na wengine 29 waliruhusiwa kurudi nyumbani.

Taarifa ya Ikulu Zanzibar jana ilieleza kuwa Dk Mwinyi alieleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuziomba familia za marehemu ziwe na subira. Dk Mwinyi kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter Dk Mwinyi aliandika “Naziomba Familia za marehemu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Inna lilahi wa inna ilayhi raji’un” Katika salamu hizo Dk Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia wizara husika itaendelea kuhakikisha waliodhurika wanaendelea kupatiwa tiba sahihi ili warudi katika hali nzuri za kiafya

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f49852897227203f05646b191557844d.jpeg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi