loader
Dk Kijaji ahimiza elimu kufanikisha sensa

Dk Kijaji ahimiza elimu kufanikisha sensa

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Ashatu Kijaji amewataka viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kuelimisha wananchi washiriki kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwakani.

Waziri Kijaji alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika yenye Kaulimbiu, "Siku ya Takwimu Afrika 2021, Kuifanya Mifumo ya Kitaifa ya Kitakwimu kuwa ya Kisasa ili kuchangia Maendeleo ya Kijamii na Kiutamaduni Barani Afrika," yaliyofanyika kitaifa wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma. 

"Viongozi mbalimbali wanatakiwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa sensa kwamba ndio chimbuko la takwimu sahihi zinazosaidia kufanya uamuzi sahihi na kupanga mipango ya maendeleo sahihi," alisema. 

DK Kijaji pia aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani watakaopita kwenye makazi yao kuwahesabu kwa kutoa takwimu sahihi badala ya kuficha baadhi ya taarifa. 

“Wananchi jitokezeni kwa wingi katika sensa itakayofanyika Agosti mwakani na mtoe ushirikiano na makarani wa sensa mtoe takwimu sahihi,” alisema. 

Dk Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini aliwaomba NBS kuwajengea uwezo wa takwimu halmashauri ili waende kutoa elimu katika ngazi za kata hadi vitongoji. 

Naye Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda alisema sensa ya mwakani isitafsiriwe tofauti wala isipotoshwe na baadhi ya watu, haina maana nyingine zaidi ya kukusanya takwimu kwa ajili ya serikali kupanga mipango yake kulingana na idadi ya wananchi wake. 

Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali (NBS), Dk Albina Chuwa alisema taasisi yake inakusanya takwimu hizo si kwa matumizi ya serikali tu, wafanyabiashara bali ni kwa ajili ya watu wote. 

Dk Chuwa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamishna ya Takwimu Barani Afrika kwa sasa alisema Siku ya Takwimu Barani Afrika ni muhimu kwani inatumika katika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa sensa ambayo ndiyo inazalisha takwimu katika kipindi cha miaka 10.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8582bf7b3d2d140e87b733324d96783c.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi