loader
World Vision yabadili kilimo cha mazoea

World Vision yabadili kilimo cha mazoea

SHIRIKA la World Vision linaendelea kutoa elimu ya kitaalamu kwenye kilimo kwa wakazi wa vijiji mbalimbali mkoani Dodoma ili kuhakikisha wanajiondoa katika kilimo cha mazoea na kuingia kwenye kilimo chenye tija. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisa Kilimo wa Kata ya Sanzawa, Salau Sumayi alisema World Vision imekuwa ikisaidia kutolewa kwa elimu ya namna ya upandaji mbegu pamoja na kuwapa mbegu bora. 

"World Vision inatusaidia sana kuwainua wakulima hawa vijijini, awali wamekuwa wakilima eneo kubwa lakini mavuno machache kwa sababu hawalimi kitaalamu," alisema Sumayi. 

Akifafanua zaidi alisema kuwa wakulima wengi hivi sasa wamekuwa wataalamu wa kilimo na kusaidia kuwafundisha wengine kulima kitaalamu ili nao wavune mazao mengi. 

Naye mratibu wa mradi wa World Vision, Joseph Kilimba alisema wako katika utekelezaji wa miradi mbalimbali mkoani Dodoma ili kuinua hali za kiuchumi za wananchi.

Alisema moja ya miradi ambayo inatekelezwa ni pamoja na ule wa Mama na mtoto lakini pia husaidia kutoa elimu ya utaalamu wa kilimo.

Alisema wamekuwa wakitoa mbegu kwa wakulima ambazo ni bora pamoja na kuwaelekeza namna ya upandaji ili waweze kupata mavuno mengi wakati wa msimu wa mavuno. 

Naye mkulima wa mazao ya chakula, Amina Mohamed kutoka Sanzawa aliishukuru World Vision kutokana na msaada wanaoutoa kwao ambao umechangia kuvuna magunia mengi. 

Amina alisema awali alikuwa akivuna gunia mbili au tatu kwa eka moja lakini hivi sasa ameongeza ekari za kulima na mwaka jana amevuna mtama gunia 32 na mahindi gunia 12. 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f4ff6a8ae5f1089563bf0e3eafd6c05c.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi