loader
Mrajis Vyama vya Ushirika, Soko Kuu Saccos wanyukana

Mrajis Vyama vya Ushirika, Soko Kuu Saccos wanyukana

MRAJIS wa Vyama vya Ushirika nchini ameingia kwenye msuguano na Chama cha kuweka na kukopa cha Soko Kuu jijini Arusha kufuatia Mrajis huyo kufunga akaunti ya benki ya Saccos hiyo kwa muda mrefu na kusababisha Saccos hiyo kushindwa kujiendesha. 

Katika kikao kilichofanyika juzi jijini Arusha, kuliibuka mzozo mkali kati ya wanachama hao na Mrajis kiasi cha kulazimika kuitwa kwa askari polisi baada ya wanachama hao kuja juu na kuongea kwa jazba wakimtishia Mrajis. 

Wakizungumza katika kikao hicho kilichoitishwa na Mrajis wa vyama vya ushirika, chenye lengo la kupata suluhu, Mrajis wa vyama vya ushirika nchini, Dk Benson Ndiege aliwataka wanachama hao kufanya uchaguzi ili kupata viongozi wapya tofauti na waliopo ambao aliwatuhumu kwa ubadhirifu. 

Mmoja ya wanachama hao, Nestory Mkusu alidai kuwa hawapo tayari kufanya suluhu na Mrajis huyo akidai wameteseka kwa muda mrefu baada ya fedha zao kufungiwa na hivyo kushindwa hata kulipa pango la ofisi na mapato ya serikali. 

Alisema kwa sasa wamelifikisha suala lao mahakamani wakitaka mahakama imwamuru Mrajis huyo afungue akaunti yao ya benki na awalipe kiasi cha Sh milioni 200 kama fidia  ya hasara waliyoipata katika kipindi chote wakati akaunti yao ya fedha haifanyi kazi. 

Mkusu alidai kuwa tangu Mrajis afunge akaunti yao iliyopo katika benki ya CRDB Desemba 12 mwaka jana uendeshaji wa Saccos hiyo umekuwa mgumu na wamekuwa wakijiendesha kwa hasara. 

Akizungumza katika kikao hicho, Mrajis wa vyama vya ushirika nchini, Dk Benson Ndiege alisema ofisi yake imefunga akaunti ya wanachama wa Arusha soko kuu saccos kutokana na viongozi wao kukosa uaminifu na kujihusisha na ubadhirifu wa fedha za wanachama. 

Dk Ndiege alisema kuwa alikuja Arusha kupata suluhu na chama hicho na anashangaa kuona masuala ya ushirika yakifikishwa mahakamani jambo ambalo alisema lisingestahili kufikia huko. 

"Akaunti yenu tutaifungua ila lazima mzingatie kwamba mrajis ndio msimamizi mkuu wa vyama vyote vya ushiriki kikiwemo cha kwenu kwa kuwa mmesema tuache mahakama itende haki sawa ila jambo hilo linapaswa kumalizika nje ya mahakama," alisema. 

Pamoja na hayo ofisi ya Mrajis imetoa tamko kwa viongozi wa Arusha soko kuu saccos waliokuwa madarakani kutowania tena nafasi hizo kufuatia kukosa sifa za uongozi baada ya kushindwa kuitisha uchaguzi kwa muda mrefu wakati muda wao wa kukaa madarakani umeisha kama sheria zinavyoelekeza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f8f0ac1630a74e48459c2a54eb4c9620.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi