loader
Dk Mwinyi ataka wakaguzi wa ndani kufika kwenye miradi

Dk Mwinyi ataka wakaguzi wa ndani kufika kwenye miradi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesisitiza wakaguzi wa ndani kutembelea miradi kwenye utendaji badala ya kuishia kwenye vitabu.

Alisema kwa kufanya hivyo watajua matumizi ya fedha yanavyofanyika.

Dk Mwinyi alitoa rai hiyo jana Ikulu Zanzibar wakati alipokutana na ujumbe wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Zelia Njeza.

Pamoja na kutoa wito huo, Rais Dk Mwinyi aliahidi Zanzibar kufanya kazi na Taasisi hiyo ili nchi iweze kupiga hatua katika suala zima la ukaguzi wa ndani.

Aidha, Dk Mwinyi alieleza kwamba kuwepo kwa Taasisi hiyo kutasaidia wakaguzi wa ndani kupata mafunzo pamoja na kutambulika.

Sambamba na hayo, Dk Mwinyi alisisitiza juu ya suala zima la maadili katika fani ya ukaguzi wa ndani hasa ikifahamika kwamba kada hiyo ina umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali.

Mapema Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Ahmed Said alieleza umuhimu wa Taasisi hiyo katika utoaji wa mafunzo ya Ukaguzi wa Ndani.

Mapema Rais na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Njeza alitoa pongezi kwa Dk Mwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wake akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Aidha, katika maelezo yake kiongozi huyo ambaye alifuatana na wajumbe wa Taasisi hiyo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara alieleza kwamba taasisi yao iliyoanzishwa mwaka 2006 iko kisheria na inafuata taratibu zote zilizowekwa ikiwa na lengo la kuimarisha kada ya Ukaguzi wa Ndani nchini.

Njema alisisitiza kwamba iwapo nchi inataka kuimarisha suala zima la utawala bora basi ni vyema suala la ukaguzi wa ndani likapewa nafasi yake.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/626182f5c147ad8d070b5a99df567b74.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi