loader
Wanawake watakiwa kuchangamkia fedha za Covid-19

Wanawake watakiwa kuchangamkia fedha za Covid-19

WAJASIRIAMALI wanawake wametakiwa kujitokeza kuchangamkia jumla ya Sh bilioni 36 ambazo ni fedha za ahueni za kupambana na Covid-19 ambazo zimeyalenga makundi mbalimbali ikiwemo waanika dagaa, wakulima wa mwani pamoja na majongoo na kaa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais anayeshughulikia Kazi na Uwezeshaji, Khadija Khamis Rajab wakati akizungumza na waandishi wa habari akielezea fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya makundi ya wajasiriamali wakiwemo wanawake za mazao ya baharini.

Rajab amesema fedha hizo zinaratibiwa na Wizara ya Uvuvi zipo tayari na wahusika ikiwemo wanawake wanatakiwa kuzichangamkia ikiwemo kujisajili katika makundi.

Amesema kwa upande wa wakulima wa mazao ya mwani wapatao 5,000 watanufaika na fedha hizo ambao wengi wao ni wanawake waliopo vijijini sehemu ambazo  mwani unalimwa kwa wingi.

Aidha, amesema katika fedha hizo zimewalenga wakulima wa mazao ya baharini ya majongoo ya pwani wapatao 100 ambayo soko lake lipo kubwa la uhakika.

Akifafanua zaidi amesema wananchi wengi ikiwemo wa maeneo ya mwambao wa baharini bado hawajachangamkia ufugaji wa majongoo ya pwani ambayo soko lake na kipato ni kikubwa.

Amewataka wananchi kujitokeza kuunda vikundi vya wajasiriamali watakaojisajili kwa ajili ya kuchangamkia fedha za ahueni ya ugonjwa wa Covid-19 ambazo zimetengwa moja kwa moja kwa wakulima wa mazao ya baharini.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Dk Aboud Suleiman Jumbe alisema sehemu ya fedha za uchumi wa buluu zimetengwa kwa waanikaji wa dagaa wapatao 6,000 pamoja na kuwapatia vifaa vya kisasa vya kukausha samaki hao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/dc6e5c595d4b837bd9a252aa15ea5943.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi