loader
SMZ yapanga mahakimu 10 mahakama ya udhalilishaji

SMZ yapanga mahakimu 10 mahakama ya udhalilishaji

KAIMU Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Khamis Ramadhan Abdalla amesema Mahakama Kuu imeongeza jumla ya mahakimu 10 kwa ajili ya kuwezesha kasi ya kusikiliza kesi za udhalilishaji wa kijinsia.

Abdalla amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya majaji pamoja na mahakimu yaliyoandaliwa na kituo cha utetezi wa sheria na haki za binadamu ambayo ni sehemu ya kujenga uwezo kwa watendaji hao katika kutekeleza haki na sheria.

Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja mafanikio makubwa yamepatikana kwa upande wa Mahakama ikiwemo kasi ya kusikiliza kesi za udhalilishaji wa kijinsia ambazo zinatokana na kuundwa kwa mahakama ya udhalilishaji wa kijinsia.

Kwa mfano alisema zipo takwimu zinazoonesha wapo jumla ya mawakili 1,429 ikiwemo wanawake 463 pamoja na wanaume 669 ambao kazi yao ni kufuatilia kesi zinazowakabili wananchi na kuona zinasikilizwa kwa haraka.

''Mahakama Kuu ya Zanzibar tumejipanga vizuri kuhakikisha kesi za udhalilishaji wa kijinsia kupitia mahakama kuu ya ukatili zinashughulikiwa kwa haraka na ndiyo maana tumeweka mahakimu 10 wanaofanya kazi hiyo,'' alisema.

Mapema Mkurugenzi wa Mashtaka na Makosa ya Jinai (DPP), Salma Ali Khamis alisema wamejipanga kuhakikisha upelelezi wa kesi unakamilika haraka na kesi kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kutajwa.

Alisema kitendo cha kucheleweshwa kusikilizwa kesi mahakamani maana yake ni kuchelewesha haki ya mtu kusikilizwa na kutolewa maamuzi yake na hivyo kwenda kinyume cha sheria za haki ya binadamu.

Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman alisema Serikali ya Awamu ya Nane imejipambanua na kutekeleza dhana ya utawala bora ikiwemo kuhakikisha mahakama zinatekeleza majukumu yake ya haki kwa wananchi wote.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/489d807d8401e2cef5b8fcfc887e251e.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi