loader
Mahakama yakataa kupokea kielelezo kesi ya Mbowe

Mahakama yakataa kupokea kielelezo kesi ya Mbowe

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imekataa kupokea barua iliyowasilishwa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi na Shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wenzake watatu.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Joachim Tiganga.

Akitoa uamuzi huo Jaji Tiganga alianza kwa kueleza hoja za ubishani wa kisheria zilizotolewa na pande zote na baadaye akatoa ufafanuzi kuwa uamuzi wake ulizingatia hoja hizo zote zilizotolewa.

Alisema katika hoja ya utambuzi wa kielelezo ni lazima shahidi atambue kielelezo kisha aeleze vitu vya upekee vilivyomo katika kielelezo hicho.

Akifafanua hoja ya mnyororo wa umiliki, Jaji Tiganga alisema kuwa  baada ya kupitia hoja hizo alijiridhisha pasi shaka kuwa mnyororo  huo haukufuatwa  kwani kwa kuwa Shahidi  huyo yupo  chini ya Jeshi la Magereza mawakili wake walitakiwa kumjulisha mkuu wa gereza husika na  kutaka kumpatia shahidi huyo kilelezo  jambo ambalo halikuelezwa kufanyika.

Upande wa mashtaka ulipinga kupokelewa kwa barua hiyo iliyodaiwa kuandikwa na mawakili wa shahidi huyo kwenda kwa Kamanda wa Polisi wa Ilala kutaka apatiwe barua ya uhamisho wa Koplo Ricardo Msemwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay.

Shahidi huyo, Mohammed Ling'wenya ambaye ni mshtakiwa wa tatu katika kesi ya msingi wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo ndogo Novemba 26, 2021 aliomba mahakama ipokee barua hiyo kama kielelezo cha ushahidi lakini ombi hilo lilipingwa na mawakili wa  mashtaka wakisimamia hoja kadhaa ikiwemo shahidi huyo kushindwa kueleza mahakama mnyororo wa umiliki wa kilelezo hicho.

Jaji Tiganga alisema kwa kuwa hakuna ofisa yeyote wa magereza aliyehusishwa basi ni wazi shahidi ameshindwa kuonesha mnyororo wa namna kielelezo kilivyomfikia na hakuna mahali imeoneshwa kwamba shahidi alipelekewa kielelezo gerezani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a2809b37dbaa77b88006d1e67f270f5f.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi