loader
Shahidi kesi ya Sabaya aeleza kwanini zimemtoka mil 90/-

Shahidi kesi ya Sabaya aeleza kwanini zimemtoka mil 90/-

SHAHIDI wa kumi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake sita, Francis Mrosso (44) ameieleza Mahakama kuwa alitishiwa maisha na ndio maana alitoa shilingi milioni 90 kwa vijana na Sabaya waliojitambulisha kuwa wao ni maofisa wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).

Aidha, alisema wengine walijitambulisha kuwa ni Maofisa wa Usalama wa Taifa (TISS) hivyo aliingiwa hofu kubwa na kuamua kutoa kiasi hicho cha fedha. 

 

Mrosso ambaye ni mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na mwenye kumiliki gereji ya magari, alidai hayo wakati akihojiwa na Wakili wa Mshitakiwa wa Kwanza katika kesi hiyo, Lengai Ole Sabaya mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda. 

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa alipokuwa nyumbani Sombetini, Sabaya alimwambia asipotoa fedha hizo watampoteza hivyo aliingiwa na hofu ya kupotezwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi ambayo haina dhamana. 

Katika kesi hiyo, mbali na Sabaya washitakiwa wengine katika shauri hilo ni Silvester Nyengu (26), Enock Togolani (41), Watson Mwahomange (27), John Odemba, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31). 

Shahidi huyo alidai kwamba alitoa fedha hizo kwa kuwa aliyemtishia maisha ni kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na ni mteule wa Rais hivyo alipata hofu. 

 Mroso alidai mahakamani huko kwamba, akiwa katika benki ya CRDB Tawi la kwa Murombo jijini Arusha, alishindwa kumweleza Meneja na watoaji wa huduma wa benki kwa kuwa alikuwa chini ya ulinzi wa vijana wa Sabaya. 

Shahidi huyo alidai kwamba aliporwa, kushurutishwa na kulazimishwa kutoa fedha kwa kuwa hakutoa kwa hiari na ridhaa yake.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9884f927347961f2667e122e2b6678e2.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi