loader
Pablo- Kazi bado nzito

Pablo- Kazi bado nzito

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amesema kuwa licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia kwenye Kombe la Shirikisho, anaamini bado ana kazi kubwa ya kufanya katika mchezo wa marejeano Desemba 5.

Katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba wameondoka na ushindi mnono wa mabao 3-0, hivyo wanahitaji sare yoyote nchini Zambia ili kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Simba imekuwa na matokeo mazuri pindi inapocheza na timu kutoka Zambia kwani imewahi kuziondoa Mufulila Wanderers katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1979 na Nkana FC mwaka 2018 katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wawakilishi hao wa Tanzania wameangukia Kombe la Shirikisho Afrika  baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa sare ya mabao 3-3, wapinzani wao Red Arrows wamefika hatua hii baada ya kuitoa Klabu ya C. D. Primeiro de Agosto ya Angola kwa bao 1-0.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Pablo alisema amefurahishwa na uwezo wa vijana wake, walikuwa haraka na morali yao ilikuwa juu kuanzia mwanzo wa mchezo hadi mwisho huenda wangeshinda mabao manne au matano. 

“Naweza kusema nimefurahishwa ingawa siwezi kufurahi zaidi kwani huu ni mchezo wa dakika 180, tunapaswa kwenda ugenini, tunaenda kukabiliana na mpinzani mgumu ambaye ni ngumu kumkabili.” 

 “Asante kwa mashabiki ingawa hali ya hewa ilikuwa mbaya kutokana na mvua kubwa, lakini walitupa sapoti kuanzia mwanzo wa mchezo hadi mwisho tulijisikia vizuri kuwaona.”

“Katika mchezo tulijipanga vizuri lakini kutokana na mvua nyasi zilikuwa zikiteleza hivyo tukabadili mipango yetu ingawa katika mchezo unapaswa kuwa na mipango B na C iwapo utafeli mpango A,” alisema.

Naye Kocha Mkuu wa Red Arrows, Chisi Mbewe, alisema kuwa licha ya kupoteza mchezo huo kwa mabao 3-0 lakini hawezi kuutumia kuangalia makosa ya kikosi chake kwani mvua haikusapoti wao kucheza na kuharibu mipango yake.

“Siwezi kuwapongeza wapinzani wangu kwani ushindi wao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na maamuzi ya waamuzi waliochezesha na kama tunataka kuendeleza mpira wa miguu Afrika tunapaswa kuongozwa na kauli mbiu ya mchezo wa kiungwana,” alisema Mbewe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/77bc8137b8201d76f36e05c30916737b.jpeg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi