loader
Yanga kukiwasha Mbeya leo

Yanga kukiwasha Mbeya leo

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inashuka katika Uwanja wa Sokoine kuwakabili wenyeji Mbeya Kwanza.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Mbeya Kwanza hawajapoteza mchezo nyumbani hivyo kuufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa pande zote mbili.

Yanga ambao wako kileleni wakiwa na pointi 16, baada ya kucheza michezo sita katika mchezo wa leo wanawakosa wachezaji wawili, Yanick Bangala mwenye kadi tatu za njano, Yacouba Songne ambaye anasumbuliwa na majeraha na Khalid Aucho anayehofiwa kuumia kwa vile ametoka kwenye majeraha hivi karibuni. 

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani kwa kila timu kuhitaji matokeo, Mbeya Kwanza wanaoshika nafasi ya 11 wakiwa na pointi saba  watakuwa wakitafuta ushindi wao wa pili msimu huu wakati Yanga  watakuwa wakitafuta ushindi wa tano ili kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasredine Nabi alisema anaamini wanaenda kukutana na timu nzuri ambayo haijapoteza mchezo nyumbani, hivyo wanatarajia kukutana na upinzani wa hali ya juu lakini watatumia uzoefu wao kuibuka na ushindi.

"Ligi Kuu msimu huu inaushindani mkubwa lakini sisi kama timu kubwa tunaamini tunaenda kupata ushindi katika mchezo huu ambao ni muhimu kwetu kwa ajili ya michezo ijayo.

"Tumewaona Mbeya Kwanza sio timu ya kubezwa, wana kikosi kizuri chenye wachezaji wenye uwezo mzuri lakini tumejipanga kuondoka na pointi tatu katika mchezo huu ingawa tunajua itakuwa vigumu ila tunapaswa kufanya kazi ya ziada,” alisema.

Naye Kocha Mkuu wa Mbeya Kwanza, Haruna Harerimana, alisema kuwa wamejipanga kufanya vizuri kutokana na maandalizi waliyofanya kwani mara nyingi michezo mikubwa inabadili vitu vingi kuanzia kambi na maandalizi.

"Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huu, vijana wangu wako tayari kwa ajili ya mchezo huu nina imani tutaenda kufanya vizuri na kuzibakiza pointi tatu katika uwanja wa nyumbani,” alisema Harerimana.

Mchezo mwingine utakaochezwa leo utakuwa kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar, ambao wanaendelea kujikongoja katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi mbili baada ya kushuka uwanjani mara sita.

Nao Biashara United ambao wako katika nafasi ya 10 kwenye msimamo watakuwa na kazi ya ziada katika Uwanja wa Karume, kuwakaribisha Polisi Tanzania, ambao wanashika nafasi ya tano.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/eb72256e005ee1186fcb14d203ee6be7.jpeg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi