loader
Teknolojia ya nyuklia kutumika kuhifadhi mazao

Teknolojia ya nyuklia kutumika kuhifadhi mazao

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeanza ujenzi wa mtambo maalumu ambao utatumia teknolojia ya nyuklia/mionzi katika kuhifadhi vyakula na mazao ili kuyaongezea muda wa matumizi na kuzikinga dhidi ya uharibifu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Peter Ngamilo katika tamasha la mawasiliano, utalii, utamaduni na maonesho ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya malamala Igoma Jijini Mwanza.

Ngamilo amesema teknolojia ya nyuklia inayojumuisha mionzi ya gamma, Xrei na elektroni (e-beam) hunurisha bidhaa mbalimbali za mazao ya kilimo, viwandani na vifaa vya matibabu ili kuua vijidudu viharibidu na kuimarisha ubora wa bidhaa. 

"Teknolojia hii ina faida kubwa katika kuboresha huduma za afya, chakula, mazao na kuboresha mazingira hivyo kuchangia ukuzaji wa uchumi wa nchi.

Vilevile Teknolojia hii pia itaweza pia kutumika kwenye bidhaa za usafi, matibabu, waya, semiconductors, vifaa vya polymeric na uponyaji/makovu ya nyuso, phytosanitary na kupunguza uchafuzi wa mazingira" amesema Ngamilo.

Ngamilo amesema Tanzania iko nyuma kulinganisha na baadhi ya nchi nyingine jirani kwa suala la kiasi na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kupelekwa nje, uongezaji wa thamani na ubora wa utengenezaji bidhaa na mazao bado umejikita katika sekta chache na kuifanya Tanzania ibaki nyuma katika ushindani wa masoko ya kimataifa.

Vyakula na vinywaji pekee ndivyo vinavyochangia karibu nusu ya usindikajii ulioongezwa thamani (value addition), wakati bidhaa za kilimo zina uongezaji wa thamani mdogo hivyo lipo hitaji la kubadilisha uchumi wetu kwa sekta zenye uchumi mdogo ili ziende kwenye uchumi mkubwa na kuongeza thamani ya bidhaa.

Aliongeza kuwa teknoljia ya nyuklia ina mchango katika mazao ya kilimo na mengineyo,
Soko la kuhifadhi mazao ya chakula duniani litakua kwa kiwango cha ukuaji wa kila mwaka wa karibu asilimia 4.8 na kuongeza kuwa,

Dhima kubwa ya kutumia teknolojia hii ni kuondoa Changamoto za kuongezeka kwa magonjwa yanayosababishwa na  wadudu wanaofanya uharibifu mkubwa wa mazao na bidhaa kabla ya kufikia mlaji, pamoja na vigezo ambavyo teknolojia hii inapewa nafasi katika kuchangia kutatua.

Mbali na hilo Ngamilo alitaja takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 30% ya vyakula duniani vinaharibika kila mwaka kwa sababu ya kuharibiwa na vijidudu au kuoza, upotevu au kuharibika kwa vyakula kuna athari kubwa katika kipato na maisha ya wakulima, na inakadiriwa  kwamba kila mwaka hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya nafaka barani Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara inafikia dola za kimarekani bilioni 4 na hii ni sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno hayo, sambamba na matukio ya binadamu kuambukizwa vijidudu vya salmonella yanafikia hadi idadi ya watu wapatao 120,000 kila mwaka ambapo maambukizi haya ya bakteria yamekuwa yakisababisha vifo vingi.

Gharama za matibabu yanayosababishwa na madhara ya maambukizi haya ya vijidudu vya salmonella na Ecoli yamekuwa yakisababisha hasara ya Dola za kimarekani bilioni 6 kila mwaka.

Teknolojia hii itachangia suluhisho la kudumu kwenye sekta ya kilimo, mifugo na  viwanda kwani teknolojia hii ni salama na ya uhakika, hakuna athari zozote zitokanazo na teknolojia hii wala chembe chembe za mionzi zinazoweza kubakia kwenye vyakula wakati wa zoezi la mnyunyurisho (Irradiation).

Hata hivyo malengo ya mradi wa tekenolojia hii ya usindikaji kwa kutumia mionzi ni pamoja na kuua vijidudu katika bidhaa na vifungashio vya vifaa vya matibabu, 

kuuawa vijidudu katika bidhaa za vyakula, nyama, samaki, viungo, matunda ama mboga mboga ili ziwe salama kwa wananchi wetu na kukubalika katika masoko ya kimataifa, kwani hhakula kilichopitishwa katika mnunurisho wa mionzi ni salama zaidi kushinda kilichopitishwa kwenye teknolojia nyingine ikiwemo kemikali.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f5a9f0b8d9643dd6185e39500180356e.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi