loader
Tanzania yajipanga kukabiliana na kirusi kipya cha corona

Tanzania yajipanga kukabiliana na kirusi kipya cha corona

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema Tanzania imejiandaa kukabiliana na kirusi kipya cha Omicron kilichogundulika Afrika Kusini hivi karibuni.

Akitoa tamko la Serikali dhidi ya mwenendo wa magonjwa mbalimbali ya mlipuko na tishio la wimbi la nne la Uviko 19 jijini Mbeya leo Novemba 30 2021, Dk Gwajima amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko 19 na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Dk Gwajima amesema takwimu zinaonyesha hadi kufikia 28 Novemba 2021 watu waliothibitika kuwa na maambukizi nchini ni 26,273 na vifo ni 731.

Akizungumzia takwimu za dunia Dk Gwajima amesema takwimu zinaonyesha hadi kufikia tarehe 29 Novemba 2021 jumla ya waliothibitika kuwa na maambukizi duniani ni 260,867,011 kati yao vifo 5,200,267

Amesema kuwa jukumu la kinga dhidi ya magonjwa yote ni la kila mwananchi ambapo Serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau wake kwa pamoja wanasimamia utekelezaji wa afua mbalimbali ili kuwezesha jamii kujikinga na Uviko 19 wakati Serikali ikiwezesha upatikanaji wa chanjo. 

Aidha, Dk Gwajima amesema kuwa Serikali imepokea chanjo ya Jansen dozi 1,227,400, Sinopharm dozi 2,578,400 na chanjo aina Pfizer, ambazo kwa ujumla wake ni 4,305,750. Amesema hadi kufikia 28 Novemba 2021 jumla ya wananchi waliopata chanjo ni 1,520,275 sawa na asilimia 2.7 ya watanzania wote.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b46db61b19717d5d2e49d20882a95384.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi