loader
Serikali kujenga vyuo vya walemavu

Serikali kujenga vyuo vya walemavu

SERIKALI imepanga kujenga na kukarabati vyuo vya watu wenye ulemavu ambapo tayari sh billion nane zimetolewa kwa ajili ya vyuo hivyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Ummy Nderiananga, katika ufunguzi wa Mradi Mpya wa “Chaguo Langu Haki Yangu ikiwa ni muendelezo wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki yake bila vikwazo ambapo tayari imetoa sh bilioni hizo nane kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha walemavu Songwe na Kigoma.

“Ipo mikakati madhubuti ya kuhakikisha masuala ya wenye ulemavu yanapewa kipaumbele ikiwamo uboreshwaji wa vyuo kikiwamo Chuo cha Mwanza ambacho kinatarajiwa kukamilika kuanzia mwezi Januari mwakani.”

“Kwasasa wizara inaratibu kwa kasi ujenzi wa vyuo vya watu wenye ulemavu na ufufuaji wa vile ambavyo vipo.

Amesema wanaendelea kufanya hivyo katika Chuo cha Yombo Dar es Salaam, na kwamba wamezindua  chuo kingine Tabora ambacho kilikuwa kimefungwa kwa miaka 10 na kumalizia ujenzi wa chuo cha kisasa Mkoa wa Tanga.

Aidha amesema serikali imeweka mkazo kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuendelea kutoa fedha ya elimu bila malipo na watu wenye ulemavu nao wananufaika.

“Serikali kupitia bohari kuu ya dawa inaendelea kuagiza mafuta ili kuwakinga dhidi ya saratani ya Ngozi kwa watu wenye ualbino sambamba na kuzitaka Halmashauri kuendelea kutenga fedha za mapato ya ndani kupitia asilimia 10 inayotolewa na kila halmashauri kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu kwa sababu hii inawasaidia kupambana na umasikini,”alieleza.

Aidha aliwataka watu wenye ulemavu kujiamini na kujisimamia katika mambo yao kwani kwa kufanya hivyo wataaminiwa zaidi na kuwataka kupendana na kuacha kupigana majungu..

Naye Mwakilishi  Mkazi wa UNFPA nchi, Jacquline Mahon amesema uzinduzi wa mradi huo  mpya wa  “Chaguo Langu Haki Yangu”, wanautekeleza kwa kwakushirikana na Ubalozi wa Finland Tanzania.

Amesema lengo  ni kuwawezesha wanawake na vijana, hasa  wasichana waliobalehe, wakiwemo wanaoishi na ulemavu, kulinda na kutunza afya na haki zao za ujinsia na uzazi na haki yao ya kuishi bila ukatili na mila kandamizi katika Mikoa ya pembezoni ikiwemo  Mara na Shinyanga kwa Tanzania Bara pamoja  na Zanzibar.

Aidha Mahon alinyesha video fupi ya kisa kifupi cha Zinduna ambaye ni mlemavu wa macho.

Zinduna hajawahi kukutana na baba yake wala mama yake kwa sababu mara nyingi mama yake anakuwa akifanya kazi shambani. Mama yake anapotoka kwenda shambani, Zinduna anafungiwa ndani ya nyumba. Dada yake anaenda shule, lakini yeye haendi. Anatumia muda mwingi kukaa nyumbani peke yake, uwezo wake bado haujatumiwa.

Amesema simulizi kama hizo ni kawaida sana nchini Tanzania  na duniani kote.

Aidha  amesema takwimu za Sensa ya Mwaka 2012 zinakadiria kuwa asilimia tisa nukta tatu ( 9.3) ya watu wa Tanzania wanaishi na ulemavu  ingawa takwimu hazijumuishi vijana au watoto wenye ulemavu.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa watu wenye ulemavu wana uwezekano mdogo wa kuhudhuria shule na kuweza kusoma na kuandika, wakati ni asilimia thelathini na nne tu (34) ya wanaume na asilimia thelathini na tani (35) ya wanawake wenye ulemavu ndio wameajiriwa; na baadhi ya watu wenye ulemavu wako nyuma zaidi.

Kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu, haswa katika maeneo ya vijijini na katika mazingira ya kibinadamu, ubaguzi wa kijinsia na ulemavu huingiliana ili kuunda vizuizi vya kikatili kwa ustawi wao, kuwaweka katika hatari ya unyanyasaji, vitendo vyenye madhara, unyanyasaji na unyonyaji.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a0ade82eb58f420113d16c6628f5aed2.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi