loader
kampuni ya udalali yaajiri vijana 200

kampuni ya udalali yaajiri vijana 200

TAKRIBANI vijana 200 wameajiriwa na Kampuni ya Udalali ya AMA’Z Auction Mart iliyopo jijini Dar es Salaam hivyo kusaidia kupunguza wimbi la vijana kukosa ajira nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Dawa Jumanne alisema hayo alipokuwa akiitambulisha kampuni hiyo mpya kwa vyombo vya habari iliyoanzishwa Julai mwaka huu.

Alisema kila mmoja anaelewa tatizo la ajira lililopo nchini, hivyo hatua ya kampuni hiyo ya kuwaajiri vijana hao italeta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema kampuni hiyo inajihusisha na kukusanya kodi na ushuru, kudai madeni, kuuza vitu mbalimbali vikiwemo nyumba, viwanja, samani, kufanya minada, kupangisha, kuratibu safari za kitalii, kukusanya taka hatarishi na kutoa ushauri wa kiufundi.

Alisema kampuni hiyo ni tofauti na nyingine zilizopo kwa kuwa katika kudai wamekuwa wakitumia ushauri zaidi kuliko kutumia nguvu kubwa, lengo ni kuwawezesha wadaiwa walioshindwa kulipa kidogo kidogo mpaka wamalize deni lao.

“Sijisikii vizuri kumwona mtu anafilisiwa kwa kuchukuliwa mali zake. Natumia ushauri zaidi kuliko vitendo,” alisema.

Alisema kampuni hiyo imedhamiria kuisaidia serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

Pia alisema wanataraji kufungua matawi katika kila Kanda nchini ikiwa ni pamoja na kujitanua nje hasa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4ba4397460f8ceb92f5420ea73bbeca6.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi