loader
Maadhimisho ya siku ya Ushindani Duniani Desemba 5

Maadhimisho ya siku ya Ushindani Duniani Desemba 5

TUME ya Ushindani wa Biashara (FCC), imesema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita imeshughulikia mashauri 19 ambapo kati ya hayo mashauri manne yalihusu washindani kula njama ya kupanga bei ili kumkandamiza mlaji.

Aidha mashauri 11 yalihusu miungano ya kampuni iliyofanywa kiholela bila kuridhiwa na tume, pamoja na mashauri manne yaliyohusiana na matumizi mabaya ya nguvu ya soko.

Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo, William Erio alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani jijini Dar es Salaam.

Alisema katika kutekeleza majukumu yake kwenye eneo la kulinda na kushajiisha ushindani katika soko la Tanzania Bara, hayo ni miongoni mwa mafanikio yaliyotokea katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.

“Tume imepewa mamlaka ya kisheria ya kusikiliza na kutolea maamuzi mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa soko la Tanzania Bara linabaki kuwa shindani.

Awali alisema msingi wa biashara yoyote ni faida hivyo katika kutengeneza faida mbinu halali, haramu na chafu pia hutumika kufikia malengo ya kibiashara ambayo ni kutengeneza faida.

“Kutokana na changamoto hii, Baraza la Umoja wa Mataifa kupitia Uamuzi namba 34/447 wa Desema 19,1979, katika kikao chake cha April inane hadi 22, 1980, kilipitisha kanuni na taratibu za kudhibiti viendo vinavyodhalilisha biashara duniani,” alisema.

Alisema kuanzia kipindi hicho kanuni hizo zimekuwa chachu ya kuundwa kwa sheria za ushindani kote ulimwenguni chini ya uratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD).

Alisema huo ndio ulikuwa msingi wa kuanzisha maadhimisho ya Siku hiyo ya Ushindani Duniani, kukumbuka kuasisiwa kwa juhudi za kudhibiti vitendo vinavyodhihirisha ushindani katika Biashara ulimwenguni ila ifikapo Disemba tano.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/20e03526217178989fd635cab29f224a.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi