loader
Gari la TFS lashambuliwa

Gari la TFS lashambuliwa

GARI la Wakala ya Huduma za Misitu (TFS) lenye namba ya usajili STL 3146, aina ya Toyota Land Cruiser limeshambuliwa kwa mawe na wananchi katika Kijiji cha Busolwa, Kata ya Nyarugusu wilayani Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo jana, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea Novemba 27 mwaka huu. Mwaibambe alisema ndani ya gari hilo kulikuwa na maofisa misitu na maofisa wanyamapori wakitokea doria na walikutana na kundi kubwa la watu waliopanga mawe barabarani.

“Kundi hilo lilikuwa likiongozwa na mkazi wa Mkolani, Joseph Ndoge (30) ambaye aliwahamasisha wenzie warushe mawe kwenye gari hilo na walifanikiwa kuvunja kioo cha mbele upande wa abiria. Ofisa wanyamapori wakati wanajihami walifyatua risasi tano lakini kundi hilo liliendelea kuwashambulia ndipo Ndoge akajeruhiwa kwa kupigwa risasi sehemu za mapajani na amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi,” alisema.

Mwaibambe aliongeza kuwa katika tukio jingine, Ofisa Wanyamapori Wilaya ya Geita, Moris Pima ameshambuliwa na watu wasiojulikana kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake. Alisema hali ya ofisa huyo inaendelea vizuri na kiini cha tukio hilo ni kujichukulia sheria mkononi kwa baadhi ya vijana wenye tabia ya kuvamia hifadhi na kuharibu misitu.

“Katika eneo la tukio yameokotwa maganda sita ya risasi, panga moja na pikipiki mbili MC.919 CCQ na haina namba za usajili aina ya SANLG na msako mkali unaendelea kuwatafuta watuhumiwa waliotenda matukio hayo,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/35c68813bbaa1efc1a3f8fd82e5e252b.jpeg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Na Yohana Shida, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi