loader
Mawaziri EAC watangaza upya ajira

Mawaziri EAC watangaza upya ajira

BARAZA la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), limetangaza kuendelea kwa mchakato wa ajira kwa nafasi zilizositishwa Oktoba mwaka huu huku wakitangaza upya baadhi ya nafasi za ajira.

Wameeleza kuwa ili kuhakikisha kunakuwa na usawa katika ajira kwa nchi wanachama, nafasi 11 za kazi zitatengwa mahususi kwa ajili ya Sudan Kusini.

Katika mchakato huo utakaoendelea Januari mwakani, Baraza limeitaka Sekretarieti ya EAC kutangaza upya nafasi ambazo walioitwa kwenye usahili walitoka nchi moja mwanachama pamoja na kutangaza upya nafasi ambayo mtu mmoja pekee ndiye aliyeitwa kwenye usaili.

Taarifa kutoka EAC inaeleza kuwa, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la EAC ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Mawaziri wa EAC na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya, Adan Mohamed, alisema waombaji walioteuliwa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watapokea mialiko kutoka Sekretarieti hivi karibuni ili kuitwa kwenye usaili.

Katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita, Baraza la Mawaziri liliiagiza Sekretarieti kutangaza tena nafasi tatu za Uganda, ambazo ni mhariri wa hansard; mwandishi wa hansard na karani msaidizi mwandamizi.

Kuhusu michango ya nchi wanachama kwa EAC, Baraza lilizitaka nchi wanachama kutoa michango yao kwa Mwaka wa Fedha wa 2021/2022 kwa mujibu wa Kanuni za Fedha za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2012, ili kuwezesha utekelezaji wa bajeti iliyoidhinishwa kwa wakati.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/acacb48eb6d1e9ea04ab8510fc318fd4.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi