loader
Wakazi Ukerewe, Mbinga watakata NMB Bonge la Mpango

Wakazi Ukerewe, Mbinga watakata NMB Bonge la Mpango

DROO ya 8 ya Kampeni ya 'NMB Bonge la Mpango - 2merudi Tena', imefanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha, ambako Theofrida Masudi wa Nansio Ukerewe na Haikamesia Mcharo wa Mbinga, Ruvuma waliibuka washindi wa pikipiki za miguu mitatu aina ya Skymark.

Bonge la Mpango ni kampeni ya miezi mitatu inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikilenga kuhamasisha utamaduni chanya wa kuweka akiba, ambako kila wiki washindi 12 hupatikana, 10 kati yao huzawadiwa pesa taslimu, huku wawili waliibuka na Skymark zenye thamani ya Sh mil 4.5 kila moja.

Katika droo hiyo iliyofanyika Ofisi za NMB Tawi la Clock Tower, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ilishuhudiwa wateja wa mikoani wakiendelea kutikisa kampeni hiyo kwa kuibuka na zawadi kubwa za Skymark kwa wiki ya nne mfululizo, tangu mshindi wa Dar es Salaam alipopatikana kwenye droo ya nne.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper, alisema washindi hao 12 waliopatikana katika droo hiyo, ni mfululizo wa wateja walionufaika na kampeni hiyo, ambayo itafikia ukomo mwishoni mwa mwezi huu wa Desemba.

Dismas aliwataja wateja ukiondoa Theofrida na Haikamesia waliojishindia Skymark, washindi wa pesa taslimu waliopatikana katika droo hiyo ya 8 (na matawi yao kwenye mabano) ni pamoja na Calvalina Stephani (Magomeni), Adeodatha Raphael (Mpanda) na Saidi Ligongo (Kibiti).

Wengine ni Floriana Mcharo (Mwenge), Deus Masai (Sengerema), Gaundence Mwakitaku (Nelson Mandela), Essay Kapia (Kambarage), Morin Msukwa (Mbozi), Faruki Bakari (Namanga) na Faraja Kusasula (Temeke).

Aidha, Meneja Mahusiano Amana za Wateja wa NMB, Monica Job, amesema washindi 12 waliopatikana katika droo ya nane, wanafanya idadi ya wanufaika wa Bonge la Mpango kufikia 99, kati yao 80 wakijinyakulia pesa taslimu na 19 wakibeba pikipiki za Skymark.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/203917b63c6255f8f0df565a46ca022d.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi