loader
Franco, Nabi watunishiana misuli

Franco, Nabi watunishiana misuli

MAKOCHA wa Simba Pablo Franco na wa Yanga, Nasriddine Nabi wametambiana kushinda mechi dhidi yao kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi hii.

Simba na Yanga zinakutana kwenye mechi ya Ligi Kuu, huku kila mmoja akionekana kumkamia mwenzie.

Yanga inaonekana kujiamini zaidi dhidi ya mpinzani wake kutokana na mwenendo wa Simba tangu kuanza mzimu kutokuwa kwenye kiwango chake kama misimu minne iliyopita.

Kocha wa Simba, Pablo ambaye timu yake imefuzu hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, amesema matokeo hayo yametia chagizo kwenye mechi ya watani.

Simba ilicheza na Red Arrows ya Zambia juzi na licha ya kufungwa mabao 2-1, imetinga hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kushinda nyumbani mabao 3-0. 

Mchezo wa Jumamosi utakuwa mchezo wa nne  kwa timu hizi kukutana mwaka huu katika mashindano tofauti, Simba iliibuka na ushindi katika mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam wakati Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika ligi ya msimu uliopita na 1-0 mchezo wa Ngao ya Jamii.

Akizungumza na gazeti hili, Franco alisema kuwa licha kuwa huu utakuwa mchezo wake wa kwanza dhidi ya Yanga, anaamini utakuwa mgumu kutokana na tabia ya michezo ya watani, ugumu pia unatokana na presha iliyopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Msimu huu malengo yetu ni makubwa tunahitaji kushinda kila  mchezo ulio mbele yetu ili tuweze kutwaa mataji yote tunayoshiriki pamoja na kufika mbali katika mashindano ya Afrika ambayo tunataka kuweka rekodi,”

“Tunawaheshimu wapinzani wetu wana timu nzuri na wanafanya vizuri  naamini nina kikosi  bora kuliko wao nawaomba mashabiki waje kwa wingi kutusapoti katika mchezo huu muhimu kwetu ambao ndio utatoa nafasi ya nani ataongoza Ligi,” alisema Franco.

Naye Nabi, ameipongeza Simba kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, lakini amewataka kujiandaa na kipigo Jumamosi hii. 

Akizungumza na gazeti hili Nabi alisema, suala la Simba kufuzu makundi haliwapi presha kwani wapo kwenye maandalizi kabambe kuhakikisha wanachukua pointi zote tatu watakapokutana. 

“Niwapongeze Simba walicheza vizuri mechi yao ya ugenini na kutimiza lengo lao ambalo ilikuwa ni kufuzu hatua ya makundi lakini mimi na wachezaji wangu tumeona mbinu zao tunajiandaa kuwa bora zaidi kwenye mchezo wetu ujao lengo ni kuchukua pointi zote tatu,” alisema Nabi.

Kocha huyo alisema anatambua kwamba hautokuwa mchezo mwepesi kwao hata kidogo kutokana na ushindi walioupata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii lakini yeye na wenzake wa benchi la ufundi wanaendelea kutumia siku zilizobaki kwa ajili ya kurekebisha mapungufu yaliyopo ili kutimiza lengo lao.

Nabi alisema pamoja na kukiamini kikosi chake lakini hawezi kuwadharau wapinzani wao Simba, kwasababu ndio mabingwa watetezi na wana wachezaji wazuri wenye uwezo wa kuwaletea shida endapo watawadharau .

Alisema anajua mechi za watani wa jadi ningumu kuzitabiri lakini yeye na jeshi lake wamejizatiti kushinda ili kutimiza mpango wao wa kumaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza na kutwaa mataji yote ya ndani msimu huu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/913cf4c533ea93e2c76c888904da0710.png

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa na Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi