loader
Tanapa yafungua msimu wa sikukuu kwa Watanzania

Tanapa yafungua msimu wa sikukuu kwa Watanzania

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka watanzania kutumia msimu huu wa sikukuu kutembelea vivutio mbalimbali zikiwemo mbuga za wanyama hatua inayolenga kuutangaza utalii wa ndani.

Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa TANAPA Kanda ya Mashariki, Steria Ndaga amesema kupitia mpango huo ujilikanao kama 'Bata loote Porini' watalii watapata fursa ya kufanya shughuli za kitalii na kuangalia wanyama pori. 

Amesema kupitia vivutio vya Hifadhi za Taifa za Mikumi, Saadan, Nyerere na Mlima Udzungwa , watalii watajifunza mambo mbalimbali yaliyopo katika mbuga hizo sambamba na tabia za wanyama, jambo litakalowafanya kufurahia.

"Kwa ujumla hifadhi hizi ni za kipekee na zaidi zipo katika maeneo ya kimkakati kwani zimepakana na miji mikubwa ya Dar e Salaam, Dodoma,Morogoro, Tanga, Iringa na Zanzibar na zinafikika kwa urahisi jambo linaloondoa usumbufu kwa watalii kuzifikia" amesema Steria

Aidha amesema kwa kuzingatia msimu huu wa sikukuu, TANAPA imeweka utaratibu wa malipo ya kutembelea hifadhi hizo  kiasi cha Sh 5000 kwa mtu mmoja huku ikiungana na Kampuni ya Nesa Africa Safari kwa wananchi wataopenda kutumia usafiri wa pamoja ambao watapaswa kuchangia.

Amesema watakaohitaji kusafiri kwa kutumia usafiri wankampuni hiyo, watapaswa kuchangai kuchangia kiasi cha Sh 70,000 siku kwa hifadhi ya Mikumi, Sh 65,000 Hifadhi ya Saadan na Sh 75,000 kwa hifhadhi ya Nyerere.

Amesema kwa mtalii atakauepemj kulala huko anapaswa kulipa gharama ya Sh 160,000 kwa hifadhi ya Mikumi, Sh 185, 000 kwa hifadhi ya Udzungwa, Sh 155,000 kwa hifadhi ya Saadan na Sh 175,000 kwa hifadhi ya Nyerere

Kwa upande wake Afisa Uhifadhi wa TANAPA,  Milima ya Udzungwa Richard Hayri alisema mbali na kujionea vivutio vya wanyama na mengineyo yaliyomo ndani ya hifadhi, hizo watalii pia watapata fursa ya kupanda mlima, kuona upepo wa maporomoko ya maji na kujifunza historia ha kale.

"Shirika limekuwa likihamasisha umma kutembelea maeneo ya hifadhi kila mara na kupelekea watanzania wengi kuwa na muamko wa kutembelea kwenye hifadhi kwa ajili ya mapumziko kama ambavyo  tumefanya hivyo tena mwaka huu" alisema Hayri

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/bb8244cb60198d18ef1d93f25522d43b.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

1 Comments

  • avatar
    yuda daniel
    08/12/2021

    sorry nilitaka kujua hzo gharama kwa kila mtu mmoja? mfano mimi mume nalipa na mke wangu analipa au nikilipa ni kwa wote?

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi