loader
Makubaliano Samia, Kenyatta yamefungua njia

Makubaliano Samia, Kenyatta yamefungua njia

NIANZE kwakutoa pongezi za dhati kwa viongozi wakuu wa Tanzania na Kenya, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Uhuru Kenyata wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwakuondoa vikwazo 46 kati ya 64 vya biashara si jambo dogo.

Kuondolewa kwa vikwazo hivyo kwa wawekezaji na wafanyabiashara na kusainiwa kwa mikataba sita, kumewajengea heshima viongozi wetu wa mataifa hayo mawili, kwani hata watakapostaafu wataacha alama lakini pia wamechangia ukuaji wa kiuchumi baina ya nchi hizo.

Ni wakati muafaka kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kuchangamkia fursa zitokanazo na kuondolewa kwa vikwazo hivyo, huku tahadhari kubwa ikitolewa kwa watendaji wa mamlaka husika kati ya nchi hizo, maana maazimio mengi na mikataba mingi inayosainiwa kati ya nchi na nchi, shida ipo chini, wakurugenzi na maofisa watendaji hususani uhamiaji na forodha.

Ninayasema haya kwasababu pamoja na kusainiwa kwa hati sita na mkataba mmoja, kuna shida kwa watendaji wa mipakani kuendekeza rushwa na urasimu, hili liangaliwe kwa jicho pevu. Nina uzoefu wa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na za SADC, baadhi ya watumishi mipakani si waadilifu wanadai rushwa na kukwamisha wafanyabiashara. Wawekezaji na wafanyabiashara watii sheria za nchi husika bila shuruti, hakuna haki bila wajibu.

Fitina za kibiashara hazinabudi kuepukwa, hatutarajii kuambiwa mahindi ya Tanzania yana sumu tena, hatutarajii kuambiwa Watanzania wamechoma vifaranga vya Wakenya laahasha, tutii mikataba, sera na sheria zilizopo katika nchi lakini tuheshimu hizi hati za makubaliano ya ushirikiano wa kimataifa pamoja na mikataba iliyosainiwa na wakuu wa nchi hizi mbili.

Hati hizo ni ya masuala ya uhamiaji, hati ya masuala ya magereza, hati ya masuala ya udhibiti wa magonjwa ya mifugo mipakani, hati ya makubaliano kuhusu masuala ya afya, nyumba na maendeleo ya makazi na hati ya masuala ya uwekezaji na mkataba wa kubadilishana wafungwa.

Ni matarajio yangu kuwa, changamoto ndogondogo zilizokuwa zikisababshwa na vikwazo vilivyoondolewa pamoja na kusainiwa hati za makubaliano na mkataba wakubadilishana wafungwa, zitapungua kama siyo kuisha kabisa.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1f7942bbd90c683b448acbde3fa9ee21.jpeg

KATIKA ukurasa wake wa habari za kimataifa ...

foto
Mwandishi: Na Dunstan Mhilu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi