loader
Minada 7 ya korosho yawaingizia wakulima Sh bil 37.3

Minada 7 ya korosho yawaingizia wakulima Sh bil 37.3

WAKULIMA wa korosho wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wanaohudumiwa na Chama kikuu cha Ushirika (Tamcu), wamepata jumla ya Sh bilioni 37.3 baada ya kuuza kilo milioni 18.1 za korosho ghafi katika minada saba.

Meneja Mkuu wa chama cha Tamcu, Imani Kalembo alisema hayo, wakati akitoa taarifa ya malipo ya fedha kwa wakulima na hali ya ununuzi wa zao la korosho kupitia minada iliyofanyika wilayani humo.

Alisema katika msimu wa mwaka 2020/2021, Tamcu imeweka malengo ya kukusanya na kuuza kilo milioni 25 za korosho na kutokana na mwenendo mzuri unaoendelea wanaweza kufikia au kuvuka kwa kuwa bado wakulima wana korosho nyingi katika maghala ya vyama vya msingi na nyingine ziko mashambani.

Alisema Tamcu ambayo inahudumia wakulima wa korosho wa wilaya ya Tunduru, Namtumbo, Songea na Nyasa katika Mkoa wa Ruvuma na wakulima kutoka Wilaya ya Ludewa mkoa jirani wa Njombe imejipanga kuhakikisha wakulima wanauza korosho zao kupitia minada na wanapata fedha zao kwa wakati.

Alisema kutokana na mikakati waliyojiwekea wamekuwa makini katika malipo na kwamba hadi sasa hakuna mkulima ambaye bado hajalipwa fedha zake. Kalembo aliwakumbusha wakulima kutambua kuwa, wakati wanaelekea mwishoni mwa msimu ni vyema wahakikishewanaingiza korosho bora ghalani ili kupata bei nzuri na kujiepusha na udanganyifu kwa kuchanganya korosho safi na chafu.

Aidha, aliwataka wakulima kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha wanazopata ikiwa ni pamoja na kuweka akiba kwani kutokana na mazingira yaliyopo waepuke kutumia katika anasa, badala yake waweke kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa kilimo. Hata hivyo, alieleza kuwa changamoto kubwa katika ukusanyaji wa korosho ni upatikanaji wa magunia, kutokana na kampuni ya Inter Bulk iliyopewa kazi ya kutengeneza kushindwa kufikia idadi ya mahitaji yao.

Alisema mahitaji ya magunia kwa ajili ya wakulima wa korosho wanaohudumiwa na Tamcu ni 800,000 na walishampata mzabuni wa kutengeneza lakini kwa bahati mbaya mzabuni huyo ameshindwa kuzalisha magunia mengi. Hata hivyo, baadhi ya wakulima wa korosho, wameiomba serikali kusaidia kuimarisha bei ya korosho kwani wanayouza kwa sasa ni ndogo ambayo hailingani na gharama za uzalishaji.

Kanyenda Hassan alisema, kilimo cha korosho kina changamoto nyingi na kubwa ikiwemo kupanda kwa bei za pembejeo zinazouzwa na ili mkulima aweze kupata mavuno analazimika kutumia zaidi ya Sh 300,000 kwa ekari moja.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/3f705fa4ae7ff5cc23259240f7571fc1.jpeg

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Na Muhidin Amri, Tunduru

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi