loader
Ndaki ataka wafugaji kurasimisha maeneo ya uchungaji

Ndaki ataka wafugaji kurasimisha maeneo ya uchungaji

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewahimiza wafugaji kuwa na maeneo ya kulishia mifugo yao jambo ambalo litawapunguzia migogoro inayowakumba kila uchao.

Waziri Ndaki alitoa wito huo alipozungumza na wafugaji wa Vijiji vya Luhembela na Masumbwe vilivyopo wilayani Mbogwe, mkoani Geita Desemba 15, mwaka huu.

“Wafugaji tukumbuke kwamba maeneo mengi tunayotumia kuchungia mifugo yetu ni maeneo huria yanayomilikiwa na serikali, lakini ni vizuri sasa tukaanza kuwa na maeneo yetu na tuyalinde kisheria kwa kuyakatia hati ya kimila au ya kawaida,” alisema.

Alisema kuwa haiwezekani mfugaji awe na ng’ombe 1,000 halafu eneo la kuchungia hana, huo ndio mwanzo wa mihangaiko na kuingia katika migogoro na watumiaji wengine wa ardhi hususani wakulima. “Sisi serikali tutawasaidia, maeneo hayo mtakayoyanunua yarasimisheni, yakatieni hati ili yawe ya kwenu, angalau uwe na eneo la kuanzia ili hata unapoiambia serikali kuhusu malisho una eneo la kwako la kuanzia,” alisisitiza.

Aliongeza kwa kusema kuwa endapo wafugaji wataendelea kufuga kwa kutegemea maeneo huria wataendelea kuwa katika migogoro na itafika mahala watakosa pa kuchungia na hatimaye watawauza ng’ombe wote.

Awali, Mfugaji wa Kijiji cha Luhembela, Maisha Magenya alimueleza Waziri Ndaki kuwa wanahitaji kuendelea kufuga lakini wanakosa elimu ya namna bora ya ufugaji kwa sababu ya uhaba wa wataalamu katika wilaya yao

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/14cf4c1108a1079878085663e63f5d11.jpeg

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Maalumu, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi