loader
AFYA ZA WACHEZAJI SIMBA ZAIMARIKA

AFYA ZA WACHEZAJI SIMBA ZAIMARIKA

MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema wachezaji wa timu hiyo waliopata ugonjwa wa mafua makali wanaendelea vizuri na baadhi yao wameanza mazoezi kujiandaa na mashindano mbalimbali yanayowakabili.

Simba ilishindwa kucheza dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi iliyopita kutokana na wachezaji wake 16 kukumbwa na ugonjwa wa mafua makali na kusababisha mchezo huo kuahirishwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mangungu alisema yeye na viongozi wenzake wamefanya jitihada za haraka kutafuta madaktari wataalamu kwa kushirikiana na madaktari wa timu yao kuhakikisha wachezaji wanapata tiba madhubuti ili warudi katika hali zao za kawaida na kuendelea na majukumu yao.

“Nafurahi kuona juhudi zetu zimezaa matunda kwa sababu baadhi tayari afya zao zimeanza kurudi katika hali ya kawaida na wengine wanaendelea na tiba, naamini mpaka kufikia katikati ya wiki hii timu nzima itakuwa sawa na kuendelea na mechi zinazotukabili,” alisema Mangungu.

Alisema hawakupenda timu yao ishindwe kucheza mechi yao na Kagera Sugar sababu ni hasara kubwa kusafirisha timu kwenda Bukoba na kushindwa kucheza lakini hawakuwa na namna.

Pia Mangungu alizungumzia dirisha dogo la usajili ambalo kwa sasa limefunguliwa na kusema uongozi umepanga kukutana na Kocha Mkuu, Pablo Franco baada ya timu kurudi Dar es Salaam wakitokea Bukoba ili kupendekeza wache

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0bc12c1aaaadd054cd4dc6dc0c48e907.jpeg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi