loader
2022 uwe mwaka wa kuchapa kazi zaidi

2022 uwe mwaka wa kuchapa kazi zaidi

SIKUKUU ya Krismasi imemalizika na kwa sasa kilicho mbele ni kusubiri kusheherekea Sikukuu ya Mwaka Mpya ambayo mkesha wake unatakuwa Ijumaa ijayo kuamkia Jumamosi.

Kama ilivyokuwa katika mkesha wa Krismasi, mkesha wa Mwaka Mpya pia imezoeleka kupata nasaha mbalimbali kutoka kwa viongozi wetu wa dini kwa wale wanaokwenda moja kwa moja katika nyumba za ibada au wanaofuatilia kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Yapo mambo mengi yameongelewa na viongozi hao katika mkesha wa Krismasi ikiwamo rai kwa vyombo vya dola, Mahakama kutenda haki, suala la kudumisha amani na upendo, kuhimiza wananchi kuchapakazi na mengineyo mengi zikiwamo pongezi kwa Rais Samia Suluhu 

Hassan kwa utendaji wake mzuri.

Kimsingi, hayo na mengine mengi kutoka kwa viongozi hao wa kiroho dhamira yake ni kuona Watanzania kwa umoja wetu tunaishi katika misingi ya amani, kupendana na kujiepusha na chuki ambazo matokeo yake ni kutengana na kuvuruga amani iliyopo nchini.

Nasema hivyo kwa kuwa yapo mataifa mengi ulimwenguni watu wake wanaishi kwa hofu kila uchao kutokana na kutoweka kwa amani miongoni mwao, huku baadhi wakipigana wao kwa wao, jambo ambalo madhara yake ni makubwa huku waathirika wakuu wakiwa ni wanawake, watoto, walemavu, wazee na wagonjwa.

Tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961, imeendelea kujichukulia sifa kutoka mataifa mbalimbali kutokana na kujaliwa utulivu mkubwa wa watu wake licha ya kuwa na makabila zaidi ya 120 huku wakiishi kwa kuaminiani kama kwamba ni kabila moja.

Nikirejea katika rai za viongozi wa dini, napenda nisisitize kwa wote walioguswa katika hotuba za viongozi hao hususan vyombo vya dola na mahakama kuona kuna haja ya wao kubadilika kutokana na ukweli kuwa kumekuwa na malalamiko mengi yanayotolewa na wananchi dhidi yao.

Ieleweke wazi kuwa, kutotenda haki hakubaki kuwa maumivu pekee kwa wale wanaowatendea, bali kundi kubwa la watu wakiwemo ndugu, jamaa pamoja na marafiki waliopo nyuma ya watu hao, hivyo jambo jema ni kuhakikisha wanatoa haki bila kuegemea upande wowote kwa maslahi ya upande fulani.

Ikumbukwe kuwa hata Rais Samia alishawahi kulisisitiza jambo hilo kwa Jeshi la Polisi hivi karibuni alipokuwa akizungumza baada ya kuwatunuku vyeo baadhi ya askari baada ya kuhitimu mafunzo, ambapo alisema hata yeye ni muathirika wa manyanyaso ya polisi.

Nia yangu siyo kuvinyooshea kidole taasisi hizo kuwa hazitendi haki, la hasha, ila ukiona malalamiko mengi yanatolewa kuzihusu basi ni wazi kuna tatizo limejificha mahali kwa baadhi ya watu waliomo ndani yake hivyo ni vyema wakafichuliwa na kuadabishwa ili kulisafisha jeshi hilo.

Rai yangu kwa jamii ni kuwa, wakati huu tunapojiandaa kusheherekea Sikukuu ya Mwaka Mpya, yatupasa kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini na kujipanga kuuanza mwaka mpya kwa kishindo kwa kuchapa kazi kwa bidii na maarifa ili kuunga mkono kauli ya Rais wetu Ramia Suluhu Hassan ya ‘Kazi Iendelee.’

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/10d6a686d05872ce420c3fd5440be701.jpeg

SERIKALI kupitia Shirika ...

foto
Mwandishi: a Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi