loader
Covid-19 yasababisha NEC kuahirisha uchaguzi Kigali

Covid-19 yasababisha NEC kuahirisha uchaguzi Kigali

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 30, mwaka huu kujaza nafasi za Baraza la Ushauri katika Jiji la Kigali kutokana na kukithiri kwa visa vya Covid-19.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NEC, uwasilishaji wa wagombea pia umefutwa hadi hapo baadaye

Katibu Mtendaji wa NEC, Charles Munyaneza, alisema uchaguzi ulioahirishwa ulipaswa kufanyika katika ngazi mbili.

“La kwanza lilikuwa ni kuwapigia kura watu wawili katika Baraza la Ushauri la Wilaya ya Nyarugenge, ambao baadaye wataingia kwenye halmashauri ya jiji, na jiji pia lilikuwa linakwenda kumpigia kura

Makamu Meya Mfawidhi wa Masuala ya Kijamii,” alisema Munyaneza.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji huyo wa NEC, Tume itaendelea kutathmini hali hiyo na watatangaza tarehe nyingine ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Kutokana na mageuzi yaliyopitishwa Mwaka 2019,

uchaguzi wa serikali za mitaa haukufanyika katika Jiji la Kigali kwa sababu hakukuwa na madiwani wa kupiga kura.

Hata hivyo, uchaguzi huo utafanyika mwaka 2024 viongozi wa eneo hilo watakapokuwa wamemaliza muhula wao wa miaka 5 ulioanza mwaka 2019.

Uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wilaya 27 zilizosalia nchini ulikamilika kwa mafanikio Novemba 26.

Katika siku za hivi karibuni, serikali imeimarisha hatua za kuzuia Covid-19 kufuatia kuzuka kwa kirusi aina ya Omicron kinachosemekana kuenea haraka kuliko kirusi cha Delta.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9b43a0e973b4a62935e03a38718d3dbb.jpeg

Kiongozi wa Azimio la Umoja ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi