loader
Wanaotaka fedha za miradi watozwe wananchi si sawa

Wanaotaka fedha za miradi watozwe wananchi si sawa

RAIS Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kuwa serikali yake itatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa kutumia fedha za mikopo yenye masharti nafuu na kamwe haitatoza wananchi kwa ajili ya kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo.

Wataalamu wa masuala ya fedha na uchumi kama Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga alimuelewa Rais Samia na wakati alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds juzi, alisema matumizi ya kodi za ndani ni gharama kwa wananchi.

“Ukitumia fedha za ndani peke yake kutekeleza miradi mikubwa utapandisha kodi, utawafanya wananchi wachangie kwa njia nyingine ambayo ni gharama kwao,” alisema Profesa Luoga.

Kauli ya Gavana imezidi kufafanua malengo ya Rais Samia kuwa hataki kuwalim-

bikizia mizigo mikubwa wananchi na kuwafanya waishi maisha magumu kama vile Tanzania siyo nchi yao kwa kuwaepushia gharama kwa kukataa kutegemea makusanyo ya ndani kugharamia miradi mikubwa.

Rais Samia kukataa kuwatoza wananchi ili kujenga miradi ya kimkakati kama vile Reli ya Kisasa (SGR), amenusuru kupandishwa kwa kodi katika maeneo mbalimbali ambazo wananchi ndio wangelipa hali ambayo ingewaumiza.

Kumbe Rais Samia kukataa kutumia tozo na kodi za ndani kulipa gharama za miradi mikubwa kama Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Nyerere amefanya maamuzi ya kutopandisha gharama za vyakula ambazo zingepanda mara dufu kama kodi ingeongezeka.

Kumbe kitendo cha Rais Samia kukataa kuwatoza wananchi fedha za kujenga miundombinu ya miradi mikubwa kama ujenzi wa Daraja la Busisi na ujenzi wa Daraja la Baharini la Tanzanite amewasaidia wananchi kutopandishiwa nauli hali ambayo ingekuwa mzigo

mkubwa kwao.

Watanzania wanaomkosoa Rais Samia kwa kuchukua maamuzi yenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi kwa kugusa mifuko yao, ina maana hawayaoni hayo manufaa wanayopata wananchi mpaka wasimame kidete kutaka wananchi watozwe kodi zaidi ili kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati?

Jibu la swali hilo ni kwamba wanajua fika madhara ambayo yangewafika wananchi ikiwa Rais angeamua kutumia kodi na tozo za ndani kugharamia miradi ya kimkakati inayohitaji matrilioni ya fedha ili kukamilika kwake.

Kama jibu ni hilo, ninaweza kusema kuwa watu hawa wanaopinga hatua ya Rais Samia kukataa kuwatoza wananchi ili kujenga miradi mikubwa na badala yake akaamua kuchukua mikopo ya masharti nafuu ili kuharakisha ujenzi wa miundombinu, wana jambo lao rohoni sio bure.

Bila shaka watu hao wanaamua kupingana na Rais kwa ajili ya kujipatia umaarufu, huku wakilenga

Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025, ndio maana baadhi ya wakosoaji hao walithubutu kutamka katika ndimi zao kuwa wananchi wafikirie kama watautoa uongozi uliopo sasa na kuingiza mwingine au watauacha uongozi wa sasa uendelee kuwa madarakani.

Kauli kama hizo zinaonesha nia ovu iliyopo katika mioyo ya viongozi hao ya kujaribu kujenga mazingira kuwashawishi wananchi kutoichagua serikali ya sasa pindi watakapoamua kugomnbea tena mwaka 2025.

Nawashauri wananchi wenzangu kuwapuuza watu hao wasiolitakia mema taifa letu kwa sababu wanatumia uhuru wa kidemokrasia ambao umeletwa na Rais Samia Suluhu Hassan kumpinga.

Watu hao hao hawakuthubutu kunyanyua midomo yao huko nyuma kupinga kile kilichofanyika ambacho hawakukubaliana nacho.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/45bcf418ecda63e4a629e7b1bc118f02.jpeg

SERIKALI kupitia Shirika ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi