loader
Tuache udhaifu, tutimize malengo 2022

Tuache udhaifu, tutimize malengo 2022

IPO kauli imezoeleka kutamkwa na kusikika masikioni mwa watu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ikiwa katika mfumo wa swali ‘Mwaka unaisha umetimiza malengo yako?’

Au mwingine anauliza ‘Mwaka unaisha umefanya nini cha kujivunia au cha maana?’

Kila mmoja anaweza kujibu kwa namna anavyopenda yeye lakini lengo likiwa ni moja tu, kutaka kujua iwapo mtu ametimiza malengo aliyokuwa amejiwekea mwanzoni mwa mwaka.

Hapo ndipo wengi wetu tunaanza kujitafakari malengo tuliyokuwa tumejiwekea tukilinganisha na yale tuliyoyatekeleza.

Wapo wanaokuwa wametekeleza kwa asilimia chache, wapo waliotekeleza kwa asilimia kubwa, pia wapo wale ambao wapowapo tu bora siku ziende wakiwa hawajafanya lolote la maana.

Hata hivyo, haijalishi nani ametekeleza vipi malengo yake ila ameweka juhudi na akili kiasi gani katika kuyatekeleza hata kama ni kwa asilimia ndogo.

Yamkini uliweka malengo makubwa ya kutekeleza katika mwaka huu, lakini kutokana na changamoto mbalimbali ukajikuta ukishindwa kuyatekeleza kwa kiwango ulichotarajia, hiyo isikuvunje moyo kwa sababu bado unayo nafasi ya kupambana na kuweka mambo sawa kwa ajili ya kufukia mashimo yaliyoachwa 2021.

Jambo la muhimu ni kuhakikisha unaweza kuchanganua na kutofautisha changamoto na madhaifu uliyonayo ambayo yamekuwa kikwazo katika kutekeleza malengo yako unayojiwekea.

Tunaposhindwa kutofautisha udhaifu tulionayo na changamoto zinazotukabili ndipo tunapopofuka na kushindwa kuziona fursa zilizopo karibu yetu na kuona kila jambo ni kubwa kuzidi uwezo wetu na hapo ndipo tunapoanza kuanguka na kushindwa kutimiza malengo na tunapokuja kushtuka mwaka umeisha na hakuna tulichofanya.

Kushindwa kutimiza malengo tuliyojiwekea 2021 kwa sababu ya udhaifu wetu kusiwe sababu au kikwazo cha kutekeleza malengo yetu mwaka 2022, bali tufanyie kazi udhaifu tulionayo ili tuweze kutimiza malengo yetu.

Si ajabu sana kumsikia mtu akisema anataka kufungua biashara hata kama ndogo lakini akilalamika hana mtaji na ni mtu huyo huyo anamiliki simu ya laki tano, huo sio mtaji? Kwanini asitumie laki moja na nusu au laki mbili kununua simu kisha hiyo inayobaki ikawa mtaji wake? Siku hizi zipo biashara hazihitaji mtaji mkubwa bali zinahitaji akili ya ubunifu na kujitoa, zipo biashara unaanza na mtaji wa Sh 35,000 na baadae ukaweza kupanua biashara yako na kukua.

Yupo mwingine anao mtaji wa fedha ya kutosha lakini anakwambia biashara ngumu, najiuliza ni biashara ipi ngumu? Mbona tunashuhudia biashara nyingi zikiendelea huko barabarani na nyingine mpya zinafunguliwa, jibu linakuja ni moja tu kushindwa kukabili udhaifu ama kwa kuendekeza uvivu au kushindwa kuumiza kichwa cha nini afanye na kikubwa zaidi ni kukosa uthubutu.

Lakini pia wakati mwingine ni kukurupuka kuanza biashara au jambo lolote bila kufanya utafiti wa kutosha, matokeo yake biashara inashindwa kuendelea na ndipo suala la biashara

“Nitoe wito kwa Watanzania kujitokeza wenyewe kwa hiari kuchanja ili kumuunga mkono Rais wetu ambaye ameonesha mfano wa kuchanja.” - Rashid Rai, Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Africa Farmers (AAFP).

ngumu linapoibuka. Hakuna namna jambo lolote litafanikiwa bila kufanyiwa utafiti na tathmini, kutokufanya hivyo pia ni udhaifu.

Mahali popote iwe kazini, nyumbani au kwenye biashara ni lazima mtu ujue udhaifu wako na ujue namna gani ya kukabiliana nao ili uweze kupiga hatua na kufanikiwa katika malengo yako, hivyo hivyo hata katika uhusiano wa kijamii ili uweze kufanikiwa kujenga uhusiano bora na wanajamii wenzako ni lazima ujue udhaifu wako na wa wenzako na namna ya kukabiliana nao.

Tukiwa tunahesabu saa kumaliza mwaka 2021, ndio wakati wa kujitafakari udhaifu wetu na kuuacha ili tufukie mashimo na kutimiza malengo tuliyojiwekea kuyatekeleza 2022.

Nawatakia heri ya mwaka mpya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/93a3ac5b69f273ec80728c1292697804.jpeg

MOJA ya misemo maarufu ya Rais mstaafu Ali Hassan ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi