loader
Tuanze mwaka kwa kuondoa vinyongo

Tuanze mwaka kwa kuondoa vinyongo

HERI ya mwaka mpya wa 2022.Kwa wale wote tuliopata neema ya kuuona mwaka huu mpya hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutupa tena nafasi ya uhai. Sio kwamba tunastahili kwa matendo yetu au juhudi zetu lakini ni huruma ya Mungu kwa wanadamu.

Mwaka 2021 kwa upande wa Tanzania ulikuwa mwaka wenye mitihani na tulipitia vipindi vigumu vya misiba, maradhi na maswahiba mengi yaliyoacha makovu kwenye mioyo ya Watanzania na kubwa zaidi ni kuondokewa na Rais Dk John Magufuli.

Mungu amrehemu! Lakini kwa upande mwingine tunapaswa kumshukuru Mungu pia kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameweka historia ya Tanzania kupata kuongozwa na rais mwanamke tena katika kipindi kigumu na chenye majonzi .

Ukiachilia hayo mwaka ulioisha ulikuwa ni mwaka uliokuwa na hofu hasa baada ya mlipuko wa virusi vya corona ulioanza Desemba 2019 na kuendelea hadi leo kuleta hofu na kupoteza wapendwa wetu.

Hata hivyo Pamoja na maradhi hayo na mengine bado kuna baadhi yetu tumeendelea kuwa na vinyongo na chuki mioyoni za mambo mbalimbali ambazo binafsi naona hazina manufaa kwa sababu hakuna anayejua kesho yake, hivyo ni vyema kuondoa vinyongo hivyo na chuki na kuanza mwaka kwa amani na watu wote.

Kwanza kwa wale wanamahesabu mwaka huu ni ule unaogawanyika hivyo kama ilivyo desturi ya wanadamu wengi tunaamini utakuwa mwaka mzuri wenye baraka, lakini kubwa zaidi kwa sote ni kujituma ,kufanya kazi kwa bidii, kufanya ibada na kuchukua tahadhari dhidi ya maradi ya corona.

Tusameheane, tuanze upya mwaka mpya, kwa wanasiasa sio vyema kuendelea kulumbana tuanze upya, tujenge nchi tuangalia katika maeneo yetu na wafuasi wetu wanamatatizo gani yanayohitaji kufanyiwa kazi badala ya kulumbana na kutupiana vijembe ambavyo kimsingi havijengi.

Yote hayo yanawezekana ikiwa kila mmoja wetu atatambua na kuwajibika kwa nafasi yake na kuacha kulaumu bali kuwa sehemu ya kutafuta suluhu.

Tuanze mwaka mpya kwa amani na upendo!

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c1287e6b9a56d84e9e484e95e1607c8f.png

SERIKALI kupitia Shirika ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi