loader
SGR kichocheo mapinduzi ya kiuchumi nchini

SGR kichocheo mapinduzi ya kiuchumi nchini

MIAKA 11 iliyopita serikali ilitunga sera ya ubia kati ya sekta binafsi na ya umma, iliyofungua milango kwa sekta binafsi kuingia ubia katika kusukuma maendeleo.

Ujio wa sera hii umekuwa kichocheo cha kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini hususani katika sekta ya uchukuzi inayojumuisha usafiri wa reli, anga, maji na reli.

Sekta ya uchukuzi ina mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii na uchumi nchini. Kwa aina za mifumo ya usafirishaji iliyopo, usafirishaji wa njia ya reli ni muhimu sana kwa wakulima na wafanyabiashara.

Nafasi ya sekta ya uchukuzi katika maendeleo ya nchi inaweza kufananishwa na damu katika mwili wa binadamu. Sekta ya uchukuzi huwezesha ukuaji wa shughuli za kiuchumi, kisiasa na kijamii kuimarika kwa wakati mmoja.

Kwa mfano wakulima wanategemea mchango wa sekta hiyo katika kusafirisha pembejeo kwenda kwenye maeneo yao ya kilimo na mazao ya kilimo kutoka kwenye maeneo ya uzalishaji kwenda kwenye masoko.

Wafanyabiashara wa viwandani huhitaji kusafirisha bidhaa zao kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda kwa watumiaji katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi; watalii huhitaji usafiri kuja nchini na kwenda kwenye maeneo mbalimbali ya vivutio vya kitalii nchini.

Mchango wa sekta ya uchukuzi kwa mujibu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika pato la taifa kwa mwaka 2010 pekee ulikuwa Sh bilioni 853.53 sawa na asilimia 5.4 ya pato la taifa.

Kati ya mwaka 2005 na 2010 sekta ya uchukuzi imekuwa kwa wastani wa asilimia 6.4 na hivyo kuwa miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi wa taifa.

Serikali pamoja na kuwa na mifumo mingi ya usafirishaji, iliona ni vyema kujenga reli ya kisasa (SGR) na kukarabati reli zilizopo. SGR kimsingi hadi kukamilika kwake itachochea ukuaji wa uchumi kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa.

SGR inayoendelea kujengwa hivi sasa, ni maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015-2020 na 2020-2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2021/22- 2025/26.

Ina umuhimu mkubwa wa kuchochea uchumi katika ngazi zote, tumeshuhudia juhudi kubwa inayofanywa na Shirika la Reli (TRC) ili kuhakikisha ujenzi wa miundombinu hiyo inakamilika ambayo inatumia fedha nyingi.

Utekelezaji wa ujenzi wa SGR unaendelea vyema kwa maeneo tofauti nchini, ambao kimsingi utakapokamilika utafungua milango ya uchumi mkubwa katika taifa hili.

Wakati anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa SGR kipande cha Mwanza - Isaka (kilometa 341) unaogharimu Sh trilioni 3.06, Rais Samia Suluhu Hassan alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa mradi huo utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kusafirisha kwa haraka na kwa kiwango kikubwa mizigo kwa mashirika, kampuni na watu binafsi.

Ujenzi huo wa reli ya kisasa mbali ya Mwanza-Isaka, unatekelezwa pia kati ya Dar es Salaam-Makutupora kwa gharama ya Sh trilioni 7.5, Dar es Salaam-Mwanza (kilometa 1,605) ambao pia ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Mwanza-Isaka unaotarajia kutengeneza ajira zaidi ya 11,000.

Mradi huu wa SGR utakapokamilika utawezesha usafirishaji wa mizigo na abiria kutoka nchini kwenda na kurudi katika nchi jirani za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

 

Kimsingi mradi huu utakapokamilika utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wafanyabiashara, wakulima na jamii yote.

KWANINI SGR Taarifa ya Wizara ya Ujenzi na uchukuzi inaeleza kuwa serikali imeendelea kuchukua hatua kuimarisha na kuendeleza sekta binafsi kwa kuandaa Sera ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), ambapo pia ni kipindi hicho cha miaka 11 serikali ilifanikiwa kuandaa muswada wa sheria ya PPP.

Kwa mujibu wa sera hiyo, taarifa ya Benki ya Dunia ya mwaka 2009 ilionesha kuwepo kwa gharama kubwa za ufanyaji wa biashara nchini kutokana na nafasi ya Tanzania kufanya biashara kushuka kutoka nafasi ya 126 kati ya nchi 183 mwaka 2008 na kushika nafasi ya 131 mwaka 2009.

Sababu ya kushuka huko kulitokana na kuongezeka vikwazo vya ufanyaji wa biashara, jambo ambalo limeanza kutafutiwa ufumbuzi ili kuwezesha huduma za usafiri kama reli ya SGR kukuza uchumi wa sekta binafsi na ule wa umma.

Kwa mfano wakulima 

wanategemea mchango wa sekta ya uchukuzi kusafirisha pembejeo katika maeneo yao ya kilimo na mazao kwenda kwenye masoko. Wafanyabiashara, viwanda na watalii hutegemea sekta hii huku reli ikiwa ni usafiri wa gharama nafuu zaidi.

HISTORIA YA RELI Uendelezaji wa reli nchini ulianzishwa kwa mara ya kwanza enzi za utawala wa Kijerumani miaka ya 1880, wakati reli ya kwanza ilipojengwa kutoka Tanga hadi Mombo mwaka 1904.

Ujenzi wa reli hiyo uliendelea na kufika Moshi mwaka 1911, na baadaye Arusha katika mwaka 1929. Ulianzia Dar es Salaam mwaka 1905 na kufika Morogoro mwaka 1907 na baadaye kufika Mwanza mwaka 1926. Reli ya Tabora hadi Kigoma ilijengwa kati ya mwaka 1912-1914.

Mtandao wote wa reli kwa wakati huo uliendelea kumilikiwa na kuendeshwa na serikali za kikoloni hadi ilipofika mwaka 1961, Tanganyika (Tanzania) ilipopata uhuru.

Kama ilivyo katika nchi nyingi duniani, usafiri wa reli umeendelea kuwa

nguzo muhimu ya kuwezesha na kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara.

Hii inatokana na ukweli kwamba usafiri wa reli ni wa gharama nafuu ikilinganishwa na aina nyingine za usafiri, hususani kwa kusafirisha mizigo mikubwa kwa umbali mrefu.

Sekta ya reli ni muhimu katika usafirishaji wa mizigo na abiria nchini. Mwaka 1984 kati ya abiria 4,100,000 waliosafiri kwa njia zote za usafiri abiria 3,040,000 walisafiri kwa reli, sawa na asilimia 74 ya abiria wote.

Katika mwaka huo pia, kati ya tani 1,030,000 za mizigo yote iliyosafirishwa nchini, tani 910,000 zilisafirishwa kwa reli, sawa na asilimia 89.

Mwaka 2002, TRC ilivunja rekodi kwa kusafirisha jumla ya tani 1,446,000 za mizigo, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa tangu mwaka 1977 shirika hilo lilipoanzishwa.

Ifahamike pia usafiri wa reli wa mizigo kwa wakulima na wananchi wa hali ya chini ni muhimu zaidi kwa sababu huongeza mnyororo wa thamani wa kiuchumi.

Kwa mfano, wizara inasema mwaka 1976 jumla ya tani 712,030 za mizigo zilisafirishwa nchini, ambapo kati ya hizo tani 698,206 sawa na asilimia 98 ilikuwa ni mizigo iliyosafirishwa kwa njia ya reli katika mifumo tofauti.

Aidha, mwaka 1987 jumla ya tani 1,000,000 ya mizigo iliweza kusafirishwa nchini, tani 902,000 zilikuwa ni mizigo iliyosafirishwa kwa njia ya reli na mwaka 1990 jumla ya tani 1,011,580 za mizigo iliweza kusafirishwa.

Kati ya tani hizo, tani 898,810 sawa na asilimia 89 ilikuwa ni mizigo iliyosafirishwa kwa njia ya reli na mwaka 2007 ni tani 545,241 ya mizigo ilisafirishwa kwa njia ya reli na kuliingizia taifa kipato cha zaidi ya Sh bilioni 200.

Usafiri wa reli ulikuwa ni sehemu ya kuwaunganisha Watanzania kufahamiana na kubadilishana tamaduni.

Pia kutokana na mwingiliano wa wageni waliokuwa wakitumia Bandari ya Mwanza kutoka nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi ilikuwa ni sehemu nzuri ya kuutangaza utalii wa ndani unaotokana na rasilimali na vivutio vya utalii vilivyopo.

SGR inayoendelea kujengwa hivi sasa, ni maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 20152020 na 2020-2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2021/222025/26.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/35a02b1ae383cc3e9c1397cd8d3be959.png

Chama cha wanafunzi wa Kike wa Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi