loader
Nigeria yafanya mabadiliko AFCON 2021

Nigeria yafanya mabadiliko AFCON 2021

SIKU tano kabla ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Cameroon kuanzia Januari 9 Nigeria imelazimika kufanya mabadiliko ya kikosi chao.

Majeraha na kushindwa kufikia makubaliano na baadhi ya klabu kumesababisha kushuka kwa idadi ya wachezaji katika kikosi hicho.

Victor Osimhen aliyepimwa na kuonekana ana virusi vya corona siku chache zilizopita na kuumia kwa Abdullahi Shehu kumesababisha mabadiliko katika orodha ya mwisho ya wacezaji 28.

Kukosekana kwa Osimhen na Henry Onyekuru anayecheza soka Ugiriki ambaye pia alikuwepo katika fainali za mwisho nchini Misri.

Kwa upande wa makipa hawajaguswa lakini kulazimishwa kukaa karantini kwa Francis Uzoho anayecheza soka nchini Cyprus, sehemu ya ulinzi na kiungo, amemuongeza Tyrone Ebuehi anayecheza Serie A katika klabu ya Venezia, Italia.

Oluwasemilogo Ajayi amerejea katika kikosi baada ya beki wa kati Leon Balogun kupata jeraha na Ajayi pia anaweza kucheza kama kiungo.

Mshambuliaji Emmanuel Dennis, ambaye klabu yake ya Ligi Kuu ya England ya Watford, imemzuia kama ilivyoelezwa na Shirikisho la Soka la Nigeria, nafasi yake imechukuliwa na mshambuliaji Peter Olayinka anayecheza soka Jamhuri ya Czec.

Fainali za 33 za Kombe la Mataifa ya Afrika zitashuhudia Super Eagles ikicheza kombe lao la nne baada ya ushindi wa mwaka 1980, 1994 na 2013. Kundi D pamoja na Misri, Sudan na Guinea-Bissau.

Watakutana na Mafarao wa Misri Januari 11 kwenye Uwanja wa Roumde Adjia kabla ya kucheza na Sudan na Guinea-Bissau tarehe 15 na 19.

Kikosi cha Nigeria

Makipa: Francis Uzoho (AC Omonia, Cyprus); John Noble (Enyimba FC); Daniel Akpeyi (Kaizer Chiefs, Afrika Kusini); Maduka Okoye (Sparta Rotterdam, Uholanzi)

Mabeki: Chidozie Awaziem (Alanyaspor FC, Uturuki); Kenneth Omeruo (CD Leganes, Spain); Oluwasemilogo Ajayi (West Bromwich Albion, England); William Ekong (Watford FC, England); Olaoluwa Aina (Torino FC, Italia); Jamilu Collins (SC Paderborn 07, Germany); Tyrone Ebuehi (Venezia FC, Italia); Zaidu Sanusi (FC Porto, Ureno); Olisa Ndah (Orlando Pirates, Afrika Kusini)

Viungo: Frank Onyeka (Brentford FC, England); Joseph Ayodele-Aribo (Glasgow Rangers, Scotland); Wilfred Ndidi (Leicester City, England); Chidera Ejuke (CSKA Moscow,Urusi); Kelechi Nwakali (SD Huesca, Hispania)

Washambuliaji: Ahmed Musa (Fatih Karagumruk, Uturuki); Samuel Chukwueze (Villarreal FC, Hispania); Henry Onyekuru (Olympiacos FC,Ugiriki); Moses Simon (FC Nantes,Ufaransa); Sadiq Umar (UD Almeria, Hispania); Taiwo Awoniyi (Union Berlin,Ujerumani);

Odion Jude Ighalo (Al-Shabab Riyadh, Saudi Arabia); Alex Iwobi (Everton FC, England); Kelechi Iheanacho (Leicester City, England); Peter Olayinka (SK Slavia Praha, Jamhuri ya Czech)

AFCON Groups

Group A: Cameroon, Burkina Faso, Ethiopia, Cape Verde

Group B: Senegal, Zimbabwe, Guinea, Malawi

Group C: Morocco, Ghana, Comoros, Gabon

Group D: Nigeria, Misri, Sudan, Guinea-Bissau

Group E: Algeria, Sierra-Leone, Equatorial Guinea, Ivory Coast

Group F: Tunisia, Mali, Mauritania, Gambia Morocco

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c9d24996810a5e7ab53ab5c39d1de45d.png

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: LAGOS, Nigeria

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi