loader
KR Mullah afiwa na baba yake

KR Mullah afiwa na baba yake

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Rashid Ziada ‘KR Mullah’ amefiwa na baba yake mzazi mkoani Lindi.

Taarifa ya kifo cha mzazi wa msanii huyo, kimeelezwa na msanii mwingine wa muziki wa kizazi kipya, Amani Temba ‘Temba’, kupitia ukurasa wake wa instagram leo.

"Pole sana KR Mullah TMK kwa kuondokewa na baba yako mzazi, Mzee Ziada, hakika kazi ya Mungu haina makosa,” ameandika Mheshimiwa Temba, ambaye pamoja na KR Mullah walitamba na kundi la TMK Wanaume Familiy.

Kwa mujibu wa Temba, msiba huo ulitokea usiku wa kuamkia leo mkoani Lindi na kuwa taratibu nyingine za mazishi zitatolewa leo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/55844acd2df99708e560c4f5be4e27e4.jpg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi