loader
Tanesco yatangaza bei mpya ya umeme

Tanesco yatangaza bei mpya ya umeme

SHIRIKA  la Umeme Tanzania (TANESCO), limetangaza gharama mpya za kuunganisha umeme, ambapo vijijini ni shilingi 27,000 kwa wateja wa njia moja bila kujali umbali wala idadi ya nguzo na kwa mjini gharama zinaanzia shilingi 272,000 kwa kutegemea umbali toka unapochukulia umeme na idadi ya nguzo.

Taarifa ya Taneso inasema kwa mteja wa mjini kuunganisha umeme  ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960 kwa mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618  umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670

Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014 kwa mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385,  umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fd8798360c163e33793d044229033464.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

2 Comments

 • avatar
  FREDY JULIUS SHONZA
  07/01/2022

  Je?kwasisi tuliolipia kabla kupanda kwa gharama,na bado utujaunganishiwa, inakuaje?

 • avatar
  Emmanuel Ishasi
  18/01/2022

  Taarifa nzuri nawaomba hii taarifa iendane kwa vitendo,tusije kufika Ofisini tukageuziwa,matangazo, Mungu ibariki Tanzania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi