loader
Hongera Zimamoto kukabiliana na majanga

Hongera Zimamoto kukabiliana na majanga

KONGOLE Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa jitihada kubwa za kukabiliana na majanga nchini.

Pongezi hizi ziwafikie kutokana na taarifa ya mwaka inayohusu kukabiliana na matukio ya moto kwa mwaka 2021 iliyotolewa juzi na Msemaji wa jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SSCF), Puyo Nzalayaimis ambayo imetoa takwimu za matukio ya kukabiliana na moto pamoja na uokozi.

Taarifa hiyo inaonesha kuwa, jeshi hilo limekabiliana na matukio ya moto 1,803 na ya uokozi 694 kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, mwaka jana katika maeneo mbalimbali.

nalipongeza jeshi hilo kwani hapo awali lilikuwa haliwezi kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu kutokana na changamoto za vifaa na utaalamu, lakini baada ya maboresho jeshi hilo limeboresha utendaji wake.

Hata hivyo, pamoja na ufanisi unaofanywa na jeshi hilo, bado ipo changamoto kwa wananchi wenyewe kuongeza umakini katika utumiaji wa baadhi ya vitu mathalani vifaa vya umeme na kusababisha matukio ya moto ambayo yangeweza kuepukika.

Ili kukabiliana na majanga ya moto yatokanayo na moto hususani unaosababishwa na hitilafu ya umeme, mfano Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), katika mfululizo wa vipindi vyake vya elimu kwa umma vinavyorushwa na Idhaa

ya Taifa (TBC Taifa) itoe muongozo wa matumizi sahihi ya vifaa vya umeme majumbani.

Shirika linapendekeza kila baada ya miaka mitano kufanyike uchunguzi wa nyaya za umeme zilizopo katika nyumba zetu ili kubaini kama zimechakaa au bado zipo katika ubora.

Lakini pia tuepukane na vifaa visivyo na ubora. Ni kweli kuwa maisha tunatofautiana kipato lakini tuwe makini kwenye mambo muhimu watu hununua nyaya za bei rahisi ambazo hazihimili changamoto za kiufundi zinapotokea.

Katika taarifa hiyo, pia imeelezwa kufanyika uokozi katika sekta ya usafiri wa majini na barabarani, huku umakini zaidi ukihitajika kwa waendesha vyombo hivyo na abiria wenyewe tuwe makini hasa pale un-

apofika bandarini na kukuta boti imejaa subiri nyingine kwani Wahenga wanasema: ‘Kawia ufike’.

Ombi langu kubwa ili kupunguza vifo vinavyotokana na vyombo vya usafiri, askari wetu waendeleze doria na kusimamia ipasavyo sheria za usalama barabarani kama walivyofanya katika sikukuu za mwisho wa mwaka, kadhalika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) liongeze bidii katika mapambano ya bidhaa bandia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/37d89c0d211db2a5f41ea61f5217dbbf.png

MOJA ya misemo maarufu ya Rais mstaafu Ali Hassan ...

foto
Mwandishi: Dunstan Mhilu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi