loader
Baraza kuimarisha Kagera Sugar

Baraza kuimarisha Kagera Sugar

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza amesema atatumia mapumziko ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuimarisha kikosi chake ili kupata matokeo mazuri itakapoanza tena.

Kagera Sugar inaburuza mkia kwenye msimamo ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza mechi 10 msimu huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Baraza alisema kinachosababisha wapate matokeo hayo ni ushindani uliopo kwenye ligi na wachezaji wake kushindwa kuzingatia mbinu anazowapa.

“Msimu huu umekuwa na ushindani mkali ikilinganishwa na uliopita, kila timu inapambana kujiweka katika mazingira salama, lakini bado tunayo nafasi ya kubadilisha mwenendo wetu ingawa tunalazimika kuwa makini,” alisema Baraza.

Alisema moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anatumia siku chache za mapumziko ya ligi kuwafua vijana wake ili itakaporejea waweze kufanya vizuri.

Alisema anajua si kazi nyepesi kutokana na ushindani uliopo, lakini Kagera ni moja ya klabu kubwa na amejipanga kutumia uwezo wake kubadili mwenendo wa timu hiyo.

Kagera Sugar kwa misimu miwili ya karibuni imekuwa na mwenendo wa kusuasua kiasi cha kucheza mechi ya mtoano msimu wa 2019/20 ili kuendelea kushiriki Ligi Kuu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/720c3681389c1ee7b86d87d178ee724d.jpeg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi