loader
Yanga yaisubiri Azam, Namungo

Yanga yaisubiri Azam, Namungo

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Yanga wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya KMKM, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar jana.

Yanga wamefikisha pointi nne katika Kundi B. Mabingwa hao walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 45, mfungaji akiwa Heritier Makambo ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na winga, Dickson Ambundo.

Yanga waliongeza bao la pili katika dakika ya 82 mfungaji akiwa Feisal Salum kwa shuti kali akimalizia pasi ya Heritier Makambo.

KMKM walipata mabao yao katika dakika ya 54, mfungaji akiwa Abdurahman Ali, ambaye alimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu wa Haji Mwinyi Ngwali, huku wakiongeza la pili katika dakika ya 92 mfungaji akiwa Abdulhalim Hamad.

Mchezo huo uliokuwa wa kumtafuta kinara wa Kundi B, ulikuwa na presha kubwa kwa pande zote mbili ambapo kila timu ilihitaji ushindi ili kutinga hatua inayofuata, hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha kuhitimisha dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakifanya mabadiliko ya wachezaji watatu kuimarisha kikosi ambapo iliwatoa Yasin Mustafa, Denis Nkane na Dickson Ambundo na nafasi zao kuchukuliwa na Jesus Moloko, Farid Musa na David Bryson.

Kocha wa KMKM, Ame Msim alifanya mabadiliko katika dakika ya 60 kwa kuwatoa Ilham Suleiman na Adam Ibrahim na nafasi zao zilichukuliwa na Mudhihir Abdallah na Joseph Yankey, kocha Cedric Kaze, alionyeshwa kadi ya njano kwa kurushiana maneno na mwamuzi wa akiba.

Hadi dakika 90 zinatamatika timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 huku Yanga ikiendelea hatua inayofuata.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ameibuka mchezaji bora wa mchezo huo na kukabidhiwa Sh 500,000.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/971ad57c9ef8dee59f4349dc818f7a18.jpeg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi