loader
BARAZA La MAWAZIRI: Watano ‘Out’ tisa wapanguliwa

BARAZA La MAWAZIRI: Watano ‘Out’ tisa wapanguliwa

RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8 Januari, 2022 amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri na nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu huku akiwaacha Mawaziri watano na kuwabadilisha wizara mawaziri wengine tisa.

Katika taarifa iliyosomwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga, Rais Samia amemfungashia virago aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Paramagamba Kabudi, William Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Geofrey Mwambe (Viwanda na Biashara), Kitilla Mkumbo ( Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji) na Mwita Waitara ( Ujenzi na Uchukuzi).

Mawaziri waliobadilishiwa wizara ni  Jenista Mhagama ambaye alikuwa Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge kueleke Ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi na Utawala bora.

Amemhamisha Ummy Mwalimu ambaye alikuwa Ofisi ya Rais Tamisemi kwenda wazara ya Afya, George Simbachawene ametoka wizara ya mambo ya ndani kwenda wizara ya katiba na sheria Profesa Joyce Ndalichako ametoka wizara ya elimu, sayasi na Tekonolojia kwenda kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu.


Pia, Rais Samia amemhamisha Innocent Bashungwa kutoka wizara ya utamaduni, sanaa na michezo na sasa atahamia ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) huku Prof. Adolf Mkenda ambaye alikuwa waziri wa kilimo ameelekea wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Dk. Dorothy Gwajima ambaye alikuwa wizara ya afya sasa atakwenda wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na wenye mahitaji maalum wakati Mohamed Omar Mchengerwa ambaye alikuwa ofisi ya rais menejimenti, utumishi  wa umma na utawala bora amehamishwa na kuwa Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9c414657a6b9c7b0e178167e1e5b8203.jpeg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Na VICKY KIMARO

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi