loader
Juhudi za serikali sekta madini zapaisha uchumi Mwanza

Juhudi za serikali sekta madini zapaisha uchumi Mwanza

MCHANGO wa sekta ya madini kwenye pato la taifa hapa nchini umezidi kuongezeka kutoka asilimia 6.7 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 7.7 kwa mwaka jana (2021) lengo la serikali likiwa ni kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

Ukuaji huu wa sekta ya madini unatokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na serikali ili kuwawezesha wananchi wake na taifa kwa ujumla kunufaika na raslimali za madini zilizopo nchini.

Uwekezaji huo ambao umeendelea kuzaa matunda unatokana na azma ya serikali ya kutekeleza vipaumbele muhimu vinavyotokana na baadhi ya miongozo yake kama Dira ya Maendeleo ya Taifa-2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17-2020/21, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 20152020 na Mwongozo wa Bajeti ya Serikali, ambapo kimsingi miongozo hiyo imetekelezeka kwa ufanisi ingawa bado zipo changamoto.

Lengo la utekelezaji wa vipaumbele hivyo ni kuwezesha rasilimali za nchi zinazotokana na madini zichangie kwenye Pato la Taifa, ukuaji wa uchumi sanjari na kufikia malengo ya miongozo hiyo muhimu ya nchi.

Ni kwa mantiki hiyo, serikali kupitia Tume ya Madini imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo ili waendelee kuvuna na kunufaika na rasilimali za madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini.

MKOANI MWANZA Ofisa Madini wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Maganga anasema Tume ya Madini kama lilivyo jukumu lake kisheria, imeendelea kufanya kazi kwa pamoja na wananchi na wachimbaji wa madini wa mikoa inayofanya shughuli za uchimbaji wa madini.

Kwa Mkoa wa Mwanza ambao unachimba madini ya almasi, dhahabu, madini ya viwandani na ujenzi (mawe, kokoto na mchanga), nao umeendelea kuwekewa mazingira mazuri ya wachimbaji kufanya kazi zao vyema.

UTAFUTAJI/UCHIMBAJI MADINI Mgodi wa Nyanzaga Maganga anasema Mkoa wa Mwanza una leseni ndogo 400, ambapo 261 ni za uchimbaji dhahabu, 4 amethsyt, 129 za madini ya ujenzi, 14 almasi, leseni za kati (ML) tano na leseni kubwa 47 za utafiti wa madini.

Anasema mradi wa uchimbaji madini wa Mgodi wa Nyanzaga ulioko wilayani Sengerema Desemba 13 mwaka jana ulikabidhiwa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini yenye namba za usajili SML 653/2021 ambapo mradi huo utakuwa unamilikiwa kwa ubia kati ya Nyanzaga Mining Company Limited kwa asilimia 84 ya gawio na serikali itapata asilimia 16 chini ya Kampuni tanzu ya Sotta Mining Corporation Limited.

“Mgodi upo katika hatua ya kutekeleza mpango wa makazi (resettlement) kwa jamii inayozunguka mradi huo,” anaeleza.

Anasema mgodi unao tarajia kuwa nwa miaka 12, unatarajia kutoa ajira ya watu 600 na kiasi cha dhahabu kinachotarajiwa kuwepo kwenye mgodi (mradi) huo wa Nyanzaga ni wakia milioni tatu (3.072 Moz).

Mgodi huo utakapoanza kazi utas- aidia katika kukiwezesha kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichoko Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza kupata malighafi ya dhahabu kutoka kwenye mgodi huo.

Kiwanda hicho na mtambo wake na ofisi zake mbili vilivyogharimu Sh bilioni 12.2, ambacho kilizinduliwa rasmi na Rais Samia Suluhu 

Hassan mwaka jana, kina uwezo wa kusafisha kilogramu 480 za dhahabu ambapo pia zinaweza kuongezeka hadi kilogramu 960 kwa siku kwa kiwango cha juu cha kimataifa (999.9 purity).

Kiwanda hicho pia kitaongeza mapato ya serikali kupitia mrahaba, tozo za ukaguzi na ushuru wa huduma, ajira za moja kwa moja 120 na zisizo za moja kwa moja 400.

Utawezesha pia madini mengine ambata (by products) kuainishwa na kuthaminiwa hapa nchini na Benki Kuu (BoT) kununua dhahabu na kuiwezesha nchi kuanza kuwa na amana ya dhahabu (Gold reserve).

BIASHARA YA MADINI Maganga anasema kwa mwaka 2021/22 jumla ya leseni 16 zimetolewa kwa wafanyabiashara wa kati ambao hununua dhahabu 12, almasi mbili, madini ya ujenzi 11 kwa wachimbaji wadogo na kuuza kwa wanunuzi.

Aidha, anasema zimetolewa leseni 26 kwa wafanyabiashara wakubwa(dealers) wa madini, ambapo 25 ni wa dhahabu na mmoja ni wa almasi.

“Wafanyabiashara wakubwa wote wanafanya biashara zao kwenye soko la kimataifa la madini Mwanza lililopo mtaa wa Butuja,” anasema.

Anasema miradi ya uchenjuaji madini (VAT Leanching) kwa mkoa ni 37, na idadi ya mitambo yenye leseni za uchenjuaji wa carbon zenye dhahabu( elusion processing plants) ni tano, ambapo kati yake nne zipo katika eneo la Mkuyuni jijini Mwanza na mbili zipo Misungwi.

MADUHULI Anasema ofisi yake ilifanikiwa kukusanya jumla ya Sh 2,730,798,270.23 ambayo ni sawa na asilimia 55.52 ya lengo la kukusanya Sh bilioni tano kwa mwaka wa fedha wa 2020/21.

Maganga anasema mafanikio hayo yametokana na kuanzishwa kwa Soko la Kimataifa la Madini la Mwanza ambayo yamekwenda sanjari na mikakati shirikishi iliyowekwa na uimarishaji wa usimamiaji wa udhibiti wa dhahabu kuanzia migodini ambapo dhahabu huzalishwa hadi kwenye mauzo yake.

SOKO LA MADINI MWANZA Anasema katika mwaka wa fedha 2020/21, jumla ya gramu 565,396.12 za dhahabu, gramu 13,186.18 za fedha na carat 16.2 za almasi za thamani ya Sh 68,973,712,958 zimeuzwa katika soko hilo.

Anasema kiasi cha Sh 4,138,422,777 kama mrahaba na ada ya ukaguzi ya Sh 689,737,130 vimelipwa serikalini na katika mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya gramu 254,158.14 za dhahabu, gramu 32,232.65 za fedha zenye thamani ya Sh 29,677,326,377 zimeuzwa pia katika soko la madini la Mwanza.

“Kiasi cha Sh 1,780,639,583 kama mrahaba na ada ya ukaguzi ya Sh 296,773,264 vimelipwa serikalini,” anasema Maganga.

Anasema kwa madini yanayotoka masoko ya nje ya mkoa kwa mwaka wa fedha 2020/22 jumla ya gramu 3,329,773.13 yaliyorekodiwa ya thamani ya Sh 397,714,926,762, mrabaha wa Sh 23,862,895,606 na ada ya ukaguzi Sh 3,977,149,268 vililipwa serikalini katika mikoa husika.

Kwa mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufiki Novemba 30, 2021 jumla ya gramu 1,558,138 za dhahabu za thamani ya Sh 183,970,935,755 zilirekodiwa ambapo mrabaha wa Sh 11,038,256,146 na ada ya ukaguzi Sh 1,839,709,357 vililipwa serikalini katika mikoa husika.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel anasema mkoa utaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wa madini ili kuwawezesha wachimbaji na wananchi kunufaika na rasilimali hizo.

Anawataka wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa kulitumia soko la kimataifa la madini lililoko Mwanza katika kuuza madini yake ambapo anasisitiza kuwa lina miundombinu bora na imara na mtaji katika kuihumia sekta ya madini.

Rais wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina anasema kuanza 

kazi kwa mgodi wa Nyanzaga ni jambo jema kwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa na ameupongeza uongozi wa mgodi huo kwa kuwa miongoni mwa wachimbaji wakubwa nchini wanaoanza kazi ya uzalishaji vizuri.

“Niushukuru pia uongozi wa mgodi kwa kutoa hekta 70 kwa wachimbaji wadogo hili ni jambo kubwa sana,” anasema.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga, anaishukuru serikali kwa kutoa leseni katika mgodi wa Nyanzaga na kwamba sasa serikali wilayani Sengerema iko kwenye zoezi la utambuzi wa wananchi waliokuwa wanaoishi kwenye eneo la mgodi ili watambuliwe waweze kupewa fidia.

“Zoezi la tathimini kwa sasa limefikia asilimia 80 na wananchi wanaostahili kulipwa fidia watalipwa ili kuwezesha shughuli za uchimbaji kuanza rasmi,” anasema.

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi