loader
Askofu awataka viongozi kuwatumikia wananchi

Askofu awataka viongozi kuwatumikia wananchi

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa wa Dodoma, Askofu Dk Evance Chande amewataka viongozi kuwatumikia wananchi badala ya kujivunia madaraka waliyokabidhiwa.

Amewataka kuisaidia jamii kuleta maendeleo pamoja na kudumisha amani na mshikamano. Askofu Dk Chande alisema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo waliochaguliwa katika ngazi mbalimbali ikiwamo ya wilaya, kata na vijiji, kwenye uchaguzi uliofanyika wilayani humo. Alisema viongozi wamechaguliwa kwa lengo la kuitumikia jamii na siyo kujivunia madaraka, kwani wakifanya hivyo hawatadumisha amani bali watavuruga na kuhatarisha mshikamano.

Aidha, Askofu Dk Chande alisema serikali inahitaji kupata msaada wa viongozi wa dini katika kutoa elimu ya kuimarisha amani na mshikamano ili kuleta maendeleo kwa Watanzania.

“Asilimia kubwa ya Watanzania hawawezi kugombana kwa ajili ya ukabila na udini, hii ni kutokana na amani tuliyonayo, hivyo viongozi ambao mmechaguliwa mnatakiwa kuidumisha na kuilinda amani pamoja na kuwatumikia watu,” alisema. Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa wa Dodoma, Shabani Shabani aliwataka viongozi hao waliochaguliwa kujiepusha na malumbano yasiyokuwa na tija na badala yake kusimamia maslahi ya Watanzania.

“Viongozi wa jumuiya hii mmepewa majukumu ya kulinda na kuenzi amani pamoja na kuliombea taifa, kuombea amani na mahitaji mbalimbali yanayowagusa Watanzania,” alisema. Katibu Tawala Wilaya ya Bahi, Jeremiah Mapogo akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo ofisini kwake, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wanaoutoa kwa ajili ya kudumisha amani na mshikamano. Alisema serikali inatambua mchango katika masuala mbalimbali ikiwamo amani na maendeleo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2cfb829ed179b48f15804edda65da248.jpeg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi