loader
Nalaila Kiula afariki dunia kuzikwa Singida

Nalaila Kiula afariki dunia kuzikwa Singida

ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Ujenzi mwaka 1991 hadi 1995, Nalaila Kiula (pichani) aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anatarajiwa kuzikwa mkoani Singida.

Taarifa iliyotolewa na familia ilisema mwili wa mwanasiasa huyo mkongwe upo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ukisubiri taratibu zingine za kifamilia ambazo zitatangazwa hapo baadaye na msiba upo nyumbani kwake Mikocheni Barabara ymwaka 1985 hadi 1995.

Wakati akiwa mbunge wa jimbo hilo, Kiula anakumbukwa kwa kufanikisha miradi ya maji katika vijiji vya Lyangilo na Kyengege kwa kutumia kata upepo na kuwafanya wananchi kuondokana na shida kubwa ya maji iliyokuwa ikilikabili jimbo hilo.

Baada ya taarifa za kifo cha kiongozi huyo, wananchi katika tarafa za Maayu, London na Mugundu kupitia mitandao ya kijamii wamesema watamkumbuka mbunge wao huyo wa zamani kwa kuwa ni katika kipindi chake barabara zilianza kurekebishwa na zikafaa kupitika.

Vilevile wananchi wa vijiji vya Kingu Ntalo, Mpondo na Fabiano maji yalikuwa yanatiririka kila kona kutokana na miradi ya kata upepo aliyoifanikisha na kuwa mfano wa mbunge aliyetatua shida ya maji kwa wananchi wake.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ffc4120ada388f7308fc8540cbb644e8.jpeg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi