loader
Uchimbaji wa Nikel kuanza nchini 2025

Uchimbaji wa Nikel kuanza nchini 2025

KAMPUNI ya Kabanga Nickel Limited imetangaza kuwa uchimbaji wa madini aina ya Nikeli Salfaidi ambayo yanatumika kutengeneza betri za magari yanayotumia mfumo wa umeme, utaanza mwaka 2025.

Imesema kinaendelea kwa sasa ni ujenzi wa mgodi na kiwanda cha kusafishia madini hao. Uwekezaji wa mradi huo wa uchimbaji Nikeli ambao serikali imeipa kampuni hiyo leseni ya miaka 33, una thamani ya zaidi ya Sh trilioni tatu na utatoa ajira rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 1,000 kwa Watanzania.

Akizungumza na HabariLEO jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kabanga Nikeli, Chris Showalter alisema mradi huo utaleta tija kwa Watanzania na taifa kwa sababu pia usafishaji wa madini hayo utafanywa hapa nchini katika kiwanda wanachojenga Kahama, mkoani Shinyanga.

“Tumepata leseni ya uchimbaji madini haya na ni furaha kwamba tumeingia ubia na kampuni inayoongoza duniani katika uchimbaji wa madini ya BHP ambayo imewekeza Dola za Marekani milioni 40 katika kampuni ya Kabanga Nickel inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya nikeli yanayopatikana wilayani Ngara mkoani Kagera,” alisema Showalter.

Alisema katika uwekezaji huo, kampuni ya Kabanga imewekeza Dola za Marekani milioni 1.3 ambazo ni sawa na Sh trilioni tatu na kuwa kati ya fedha hizo, Dola milioni 950 zitatumika kwenye uwekezaji wa mgodi wa Ngara, mkoani Kagera.

Alisema Dola milioni 350 kati ya fedha hizo zitatumika kujenga kiwanda cha kusafisha madini Kahama, mkoani Shinyanga ambacho kitatumika pia kusafisha madini mengine ili kuyapa thamani kabla ya kwenda kuuzwa nje.

“Tunashukuru sana mazingira ya uwekezaji nchini yanazidi kuboreka na ndio sababu ya msingi hawa kampinu ya BHP ambayo ni moja ya kampuni kubwa duniani za madini wamekubali kuingia ubia nasi na kuwekeza, wameangalia vigezo ikiwamo mazingira bora ya uwekezaji Tanzania,” alisema.

Showalter alisema hivi sasa kinachofanyika ndani ya miaka mitatu kuanzia mwaka huu ni ujenzi wa kiwanda hicho cha kusafisha madini na mgodi na baada ya kukamilika, mwaka 2025 ndio mradi utaanza kazi ya kuchimba madini hayo na kuyasafisha hapa nchini. Kuhusu ajira, Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Ubia na Serikali ya Tembo Kabanga, Benedict Busunzu alisema fursa za ajira zitakazotolewa ni zaidi ya 1,000 zikiwemo rasmi na zisizo rasmi.

Alisema pia kampuni hiyo imepanga kuweka mpango mzuri wa kusaidia wananchi wanaozunguka eneo la mradi kwa kuwahusisha kupanga vitu muhimu wanavyohitajika katika eneo hilo ili vitekelezwe ikiwemo kusaidia miradi ya ujenzi wa shule, vituo vya afya na ajira.

Awali, taarifa ya kampuni hiyo ilisema baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na BHP, wanategemea kuzalisha tani 40,000 za nikeli, tani 6,000 za shaba na tani 3,000 za kobalti kwa mwaka.

Mradi unakadiriwa utakuwa na uhai wa takribani miaka zaidi ya 30 ya utafiti na uchimbaji. Kwa uwekezaji huo, Tanzania itanufaika kikamilifu kwa uzalishaji wa madini hayo muhimu kutengenezea betri bila kutumia teknolojia ya kuyeyusha.

Serikali ya Tanzania ina asilimia 16 ya hisa kupitia kampuni ya Tembo Nickel na Kabanga Nickel Ltd ya Uingereza inamiliki hisa zilizobaki.

Katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) mjini Glasgow Novemba mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza haja ya nchi zilizoendelea kulisaidia Bara la Afrika katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Ubia kati ya Kabanga na serikali na ushirikiano kutoka BHP ni mfano wa namna ambayo azma hiyo inaweza kufikiwa.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/c7eb29f89847afd5b488e0e810c277a6.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi