loader
Mkenda kutumia wastaafu kuboresha elimu

Mkenda kutumia wastaafu kuboresha elimu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameahidi kutumia wabobezi katika sekta ya elimu wakiwamo wastaafu katika kuchangia mawazo ya kuboresha elimu nchini.

Profesa Mkenda alisema hayo jana jijini hapa wakati wa makabidhiano ya ofisi na Profesa Joyce Ndalichako ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

“Najua kwa sasa kuna kazi inaendelea ndani ya wizara ya mapitio ya mitaala. Katika kuboresha elimu ya Tanzania sitaona shida kuwatafuta wataalamu wabobezi wa elimu kukaa nao kwa nia ya kutoa mchango wao, hivyo nisisitize milango ya wizara ipo wazi kwa wataalamu kutoa maoni yao yatakayosaidia kuboresha zaidi sekta ya elimu,” alisema.

Alisema kuna mambo mengi yanahitaji kujadiliwa na wadau na wataalamu. Aliwataka wasiwe waoga kuleta wataalamu wa ndani ya nchi kutoka mahali popote.

“Kwa mfano kuna suala kuwa elimu yetu inatoa watu ambao hawaajiriki hili ni suala ambalo lazima tujadili humu ndani, lakini michakato imeshaanza, majadiliano yataendelea na najua maoni yanakusanywa kwa watu na najua jinsi gani hawaajiriki inawezekana pia uchumi unachangia,” alisema.

“Ili kuwa na ufanisi katika majukumu yetu, naomba ushirikiano na msiwe na nidhamu ya woga pale mnapoona siyo, ninyi ni wataalamu wa wizara hii. Mkiniona naenda sivyo ninyi ndio wataalamu niambieni hapa panahitajika kufanya jambo fulani na si kuanza kusema Waziri tunamuona anachanja mbuga kwingine tumuone atafika wapi, naomba tuzungumze mambo humu ndani tushauriane na kuwa na uamuzi wa pamoja wa wizara,” alisema.

Kwa upande wa Profesa Ndalichako, alisema kuhudumu kwa muda mrefu kwenye wizara hiyo kumetokana na ushirikiano aliopata kutoka kwa watendaji wake.

Alisema anakabidhi wizara kwa Profesa Mkenda ambaye hana shaka na utendaji wake. Alisisitiza kuwa anaamini waziri huyo atatekeleza kwa ufanisi mipango inayoendelea ndani ya wizara hiyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8de5b2555179ee7fb49a91dc7ae4adda.jpeg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi