loader
TLP yasaidia  akinamama,  watoto  hospitalini

TLP yasaidia akinamama, watoto hospitalini

CHAMA cha Tanzania Labour (TLP) Mkoa wa Dodoma kimeishauri serikali kuweka mkazo katika kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na afya.

Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dodoma, Damal Richard alisema hayo jana jijini hapa wakati wa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa akinamama na watoto waliolazwa katika hospitali ya rufani mkoani hapa. Damal alisema serikali inatakiwa kuweka mikakati ya kusaidia watoto waliopo katika mazingira hatarishi.

“Naomba serikali iweke mkazo katika kuwaondoa watoto wa mitaani ili waende kupata haki zao za msingi katika familia zao ikiwemo kwenda shule, malazi pamoja na matibabu kama ilivyo kwa watoto wengine,” alisema.

Alisema watoto wengi wanaozurura mitaani wanazo familia zao hivyo jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwalinda. Aliwataka akinamama kuangalia familia zao kutokana na wengi wao kuwa na shughuli nyingi.

“Akinamama wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu kuacha tabia hii ya kutupa pamoja na kutelekeza watoto na kutokomea kusikojulikana,” alisema.

Alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuwafariji akinamama hao pamoja na watoto ambao wamelazwa katika hospitali hiyo.

“Lakini hii kwetu ni kama kusherehekea mwaka mpya na wao kwa kuwapatia faraja na matumaini wakati huu wakiwa wamelazwa hospitalini ili na wao wajione kuwa pamoja na kuumwa lakini bado ni sehemu ya jamii,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6e1db24546011cccb8f2a457f1dd38a1.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi