loader
Chama arejea Msimbazi

Chama arejea Msimbazi

SIO tetesi tena, furaha kwa wanasimba imeongezeka mara mbili,  Simba imetangaza kumrejesha kiungo wao raia wa Zambia, Clatous Chama.

Chama aliachana na Simba SC, msimu uliopita na kuelekea Morocco ambako alijiunga na Berkane, baada ya mambo kwenda tofauti ameamua kurejea kwa waajiri wake wa zamani.

Simba imemtambulisha Chama kama usajili wao pekee katika dirisha hilo dogo la usajili. Furaha kwa wanasimba imekuwa mara mbili baada ya jana kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Kiungo huyo aliwahi kucheza Simba kwa mafanikio ambapo kwa msimu miwili tofauti aliiwezesha timu hiyo kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fbb579fbf90e9404a6a7aa1ec6518116.jpg

WABUNIFU na Wanamitindo wa Zanzibar wahaidi kutumia fursa ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi