loader
Dk Kashililah ajitosa Uspika wa Bunge

Dk Kashililah ajitosa Uspika wa Bunge

ALIYEKUWA Katibu wa Bunge wa Bunge, Dk ThomasKashilila amejitosa kuwnaia kinyang’anyiro cha spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tazania.

Dk Kashilillah alikuwa Katibu wa Bunge tangu mwaka 2009 hadi mwaka 2017 baada ya Hayati Rais John Magufuli kumhamisha nafasi hiyo na kumteua kuwa Naibu Katibu wa Wizara ya Kilimo, huku Stephen Kagaigai ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akiteuliwa kushika nafasi hiyo.

Leo Januari 14, 2022, Dk Kashilillah amefika katika ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM jijini Dar es Salaam na kuwa mmoja wa waliochukua fomu ya kuteuliwa na chama hicho kugombea uspika.

Dk Kashilillah amefika katika ofisi hizo za CCM saa 3:00 na kuelekea chumba cha Oganizesheni ambako fomu hizo ndipo hutolewa ili kukamilisha taratibu za kuipata ikiwemo malipo ya shilingi  milioni 1 yanayolipwa kupitia benki.

Hata hivyo, alipotoka saa 5:30, alikataa kuzungumza na waandishi waliokuwa katika eneo hilo, akisema sio wakati wake.

Zaidi ya wana CCM 50 wamechukua fomu za kugombea nafasi hiyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cfcf590a593ce4e9eedcc386029a9958.jpg

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi